AFUNGWA MIAKA 77 JELA KWA KUUA FARU.
Mtu
aliyewinda na kuua faru watatu nchini Afrika Kusini amehukumiwa kwenda
jela kwa miaka sabini na saba. Hii ni adhabu kubwa kuwahi kutolewa kwa
kosa kama hilo. Mandla Chauke aliwapiga risasi watoto wa faru katika
hifadhi ya wanyama ya Kruger mwaka 2011. Katika tukio hilo, mapigano ya
risasi yalizuka kati ya majangili hao na walinzi wa hifadhi, ambapo
mmoja wa washirika wa Chauke aliuawa, na yeye kukutwa na hatia ya mauaji
yake. Afisa mmoja wa bodi ya hifadhi za taifa Afrika Kusini amefurahia
hukumu hiyo akisema mahakama zimetambua athari za uwindaji haramu katika
uchumi unaotegemea utalii. Pembe ya faru inaweza kuuzwa kwa dola laki
moja na nusu katika masoko ya kimagenndo katika maeneo ya Asia. Watu
wengi nchini China na Vietnam wanadhani pembe hizo zina tibu maradhi
mbalimbali, ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu hilo
No comments:
Post a Comment