Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe,
akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku
waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo
hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitr,
leo, Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia
kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.
Pinda
akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho
kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina
la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo
ameyakusanya na kisha kutengeneza kitabu kwa ajili ya kukisambaza nchini
kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau
kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha
uchapishaji wa kitabu hicho.
No comments:
Post a Comment