Polisi
nchini Kenya inaeleza kwamba washambuliaji wamewauwa watu 29 huko Lamu
na Tana River. Polisi inasema wahusika wa shambulio hilo ni wanachama wa
kundi la Mombasa Republic Council-MRC ingawa kundi la wanamgambo wa
Al-Shabab kutoka Somalia linadai kuhusika.
Vyombo
vya habari vya kenya vinamnukuu naibu inspeka mkuu wa polisi Grace
Kaindi akisema jumapili kwamba watuhumiwa wakuu ni wanachama wa MRC na
kwamba malengo yao huwenda yakawa ni ya kisiasa, kikabila au suala la
mashamba. "Kundi la kiasi cha watu 30 hadi 50 waliwashambulia maafisa wa
polisi waliokua katika kituo cha polisi cha Gamba . kulikuwepo na
mashambulizi makali. Na kundi moja la washambuliaji walifanikiwa kuingia
ndani ya kituo na kuwauwa watu watano waliokua wanashikiliwa huko.
Afisa moja wa polisi aliuliwa na wawili kujeruhiwa
No comments:
Post a Comment