Wednesday, July 30, 2014

BREAKING NEWSSS:17 WAFARIKI HAPO HAPO KATIKA AJALI YA BASI LA MORO BEST DODOMA


Capture5
July 30 imesambaa Taarifa ya ajali ambayo imetokea mapema leo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ajali iliyosababisha vifo vya watu 17 kati yao wanaume 12, wanawake 5 na majeruhi kwa mujibu wa jeshi la Polisi Dodoma.

Capture4Ajali hiyo imetokea majira ya saa 08:00 asubuhi eneo la Pandambili barabara ya Dodoma –Morogoro ambayo imehusisha basi la kampuni ya Moro Best yenye namba T258 AHV ambalo lilikuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.
Capture3Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na SAID S/O LUSOGO liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na GILBERT S/O ISAYA NEMANYA.
Taarifa ya kamanda wa Polisi inasema katika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni 5. Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari lingine na kwenda kuligonga busi hilo

CHIMBUKO LA AMANI NA UTULIVU NCHINI NI DINI-MEMBE.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe, akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitr, leo, Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.

 Mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na  Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

 Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.

 Pinda akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo ameyakusanya na kisha kutengeneza kitabu kwa ajili ya kukisambaza nchini kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha uchapishaji wa kitabu hicho.

Monday, July 28, 2014

VIONGOZI WA CHUO NA HOSPITALI YA IMTU WATINGA MAHAKAMANI,DPP AWAFUTIA MASHTAKA.

 Washtakiwa wakiwa katika gari la polisi 
Washtakiwa wakisubiri kuingia mahakamani.
 
 Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), aliwapandisha kizimbani vigogo wanne wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) na baadaye kuwaondolea mashitaka kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashtaka ya kushindwa kufukia viungo vya binadamu na kupeleka hati ya kufukia viungo vilivyotumika kufundishia kwa Kampuni Coroner. 
 
 Vigogo hao ni, Venkat Subbaian (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (59) na Dinesh Kumar (27) ambao walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo  saa 8:07  mchana.  Washtakiwa hao walisimama kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kwey Lusemwa. 
 
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Magoma Magina alidai kuwa Julai 20, mwaka huu washtakiwa wakiwa na nyadhifa  tofauti, Profesa, Mtawala na wahadhiri, kwa makusudi walishindwa kufukia mifuko 83 iliyokuwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria ya 128 kifungu cha 8 na cha 9 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). 
 
 Magina alidai kuwa katika shitaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa kupeleka hati ya kumtarifu kwamba wamefukia viungo hivyo baada ya kutumika kufundishia kama sheria inavyowataka. Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja. 
 
Hata hivyo, kabla mahakama haijasikiliza kipengele cha dhamana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salum Ahmed aliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa DPP akidai kuwa anawaondolea vigogo hao mashtaka na kwamba hana nia ya kuendelea kuwashitaki. 
 
 Ahmed alidai kuwa DPP anawaondolea washtakiwa mashitaka hayo chini ya kifungu cha 91 kidogo cha (1) cha CPA kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaki. 
 
 Wakili wa washtakiwa Gaudiosus Ishengoma alisema kwamba inaonekana kuna mbinu kubwa dhidi ya washtakiwa. Alisema anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa. 
 
Alisema kutokana na sababu hiyo, ana wasiwasi kwamba inawezekana DPP ana nia ya kuwafungulia wateja wangu kesi yenye mashitaka yasiyokuwa na dhamana ili wakasote mahabusu. 
 
 Viwanja vya mahakama hiyo vilikuwa tulivu huku wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa IMTU wakiwa wamesimama katika makundi makundi wakijadiliana hili na lile. 
 
Kupitia magari ya Jeshi la Polisi, T 366 AVG aina ya Rav4 alipanda mshtakiwa wa tatu kwa madai kuwa ni mgonjwa na washtakiwa wengine waliondoka mahakamani hapo katika gari yenye namba za usajili KX06EFY aina ya Toyota Landcruiser na kurudishwa mahabusu ya jeshi hilo

Thursday, July 24, 2014

AFUNGWA MIAKA 77 JELA KWA KUUA FARU.

rhino_951a1.jpg
Mtu aliyewinda na kuua faru watatu nchini Afrika Kusini amehukumiwa kwenda jela kwa miaka sabini na saba. Hii ni adhabu kubwa kuwahi kutolewa kwa kosa kama hilo. Mandla Chauke aliwapiga risasi watoto wa faru katika hifadhi ya wanyama ya Kruger mwaka 2011. Katika tukio hilo, mapigano ya risasi yalizuka kati ya majangili hao na walinzi wa hifadhi, ambapo mmoja wa washirika wa Chauke aliuawa, na yeye kukutwa na hatia ya mauaji yake. Afisa mmoja wa bodi ya hifadhi za taifa Afrika Kusini amefurahia hukumu hiyo akisema mahakama zimetambua athari za uwindaji haramu katika uchumi unaotegemea utalii. Pembe ya faru inaweza kuuzwa kwa dola laki moja na nusu katika masoko ya kimagenndo katika maeneo ya Asia. Watu wengi nchini China na Vietnam wanadhani pembe hizo zina tibu maradhi mbalimbali, ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu hilo

Monday, July 21, 2014

BREAKING NEWS.... MAITI ZA WATU ZILIZO KAUSHWA ZAKAMATWA NDANI YA MIFUKO ENEO LA BUNJU USIKU HUU


 Mmoja ya Kiungo cha Mguu
 Baadhi ya Mifuko ambamo Maiti izo zilikuwa zimewekwa
 Moja ya kichwa cha Binadamu ambacho kimetolewa katika moja ya Mifuko hiyo
 Umati wa watu wakiwa wanashuhudia tukio hilo muda huu
 Watu zaidi wakiwa wanaongezeka katika eneo la Tukio

Mpaka tunaondoka eneo la Tukio Miili ilikuwa imechukuliwa na Jeshi la Polisi kwa Uchunguzi zaidi, Taarifa kamili italetwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam.

Thursday, July 17, 2014

MSANII WA MUZIKI AELEZA SABABU ILIYOMFANYA AKATE UUME WAKE


Je unamkumbuka mwanamuziki wa kufoka Andre Johnson ambaye alikata Uume wake mwezi Aprili na kisha kujirusha kutoka juu ya jumba moja mjini Los Angeles?
Sasa basi emetoa sababu zake akisema alikuwa na akili timamu alipokuwa anafanya hivyo.
Johnson, aliishangaza jamii ya wanamuziki wa kizazi kipya, kufuatia kitendo chake cha kukata uume wake Kaskazini mwa Hollywood mwezi Aprili. Madaktari walishindwa kunguanisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya mwili wake.
Tangu hapo alikimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.
Lakini aliamua wiki hii kujieleza kwa nini alichukua hatua hiyo na kuambia kituo cha televisheni cha E! nchini Marekani:''Ndio nilikuwa nimetumia dawa za kulevya , lakini nilikuwa najifahamu.''
'Mimi sio mwanadamu'
Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha masaibu yangu. Suluhu langu kwa masaiibu yangu ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu, 'mini ni mungu''.......''vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi. Mimi siko hapa ardhini kama mwanadamu bali mungu ''
Matamshi yake Johnson, yanaonekana kama ya mtu anayekabiliwa na matatizo ya kiakili, lakini Johnson anasisitiza kuwa yuko timamu , yeye sio kichaa.
Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini daktari alimwambia hana matatizo.
''Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo sikutaka kuongea sana kuhusu swala hilo. ''
"sikutaka kujiua ,'' alisema Johnson.''
"hilo ndilo jibu langu kwa kitendo nilichokifanya. Leo nafurahi niko hai, na hilo ndilo jambo muhimu zaidi, hata bila ya uume wangu.

MTUHUMIWA WA UGAIDI KENYA AKAMATWA TANZANIA.


Mmoja wa watuhumiwa wa matukio ya ugaidi nchini Kenya,Jihad Gaibon Swaleh, amefikishwa mahakamani nchini Tanzania.
Mshukiwa huyo amesomewa mashtaka ya kufadhili vitendo vya kigaidi nchini Kenya.
Washtakiwa wote 17 wamerejeshwa rumande baada ya kusomewa mashtaka ya vitendo vya kigadi nchini Tanzania pamoja na nchi jirani ya Kenya.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali mwandamizi Prosper Mwangamila ulidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kuwa kwa kutumia mtandao wa facebook aliweza kushawishi watu wengine kuwasiliana kwa lengo la kutafuta vifaa vya kulipua mabomu nchini Kenya na kusababisha majerahi, hofu na Vifo.
Jihand Gaibon Swaleh ambaye amesomewa mashtaka mawili hakuruhusiwa kukiri wala kukana mashitaka yanayomkabili kutokana na kwamba mashitaka hayo yanaangukia katika makosa ya ugaidi ambayo kwa mujibu wa sheria nchini Tanzania mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kuendesha kesi za namna hiyo.
Katika kesi ya awali kutajwa mahakamani hapo washtakiwa wengine 16 walisomewa mashtaka mawili ikiwemo kula njama kutenda kosa pamoja na kushawishi wenzao kushiriki katika vitendo vya kigaidi katika sehemu mbali mbali nchini Tanzania.
Ni makosa ambayo wanadaiwa kutenda kati ya Januari mwaka 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti Tanzania.
Katika kesi zote mbili dhidi ya washtakiwa hao Upande wa mashtaka uliiambia mahakama iliyokuwa chini ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo bi Hellen Riwa kuwa upelelezi bado unaendelea na hivyo kuiomba mahakama kuahirisha kesi hizo hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Julai.
Awali mapema asubuhi msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania Bi Advera John Bulimba aliwealeza waandishi wa habari kuhusu tuhuma dhidi ya washtakiwa hao
Hii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa pamoja wakikabiliwa na tuhuma za makosa ya kigaidi huku mtandao wa kijamii wa facebook nao ukitajwa kuhusika katika kutawanya taarifa za kuwezesha kutenda makosa hayo.

Wednesday, July 16, 2014

DAWA YA UKIMWI KUPATIKANA 2030-WHO

Kuna uwezekano kuwa UKIMWI unaweza kudhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa.
Shirika hilo- UNAids- limesema idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya HIV na vifo vinavyotokana na UKIMWI inapungua.
Hata hivyo, imetoa wito kwa juhudi zaidi za kimataifa kwa kuwa "kasi ya sasa haiwezi kumaliza ugonjwa huo".
Shirika la Madaktari wasio na Mipaka limeonya kuwa wengi wa watu wanaohitaji dawa za kufubaza virusi vya HIV, bado hawawezi kuzipata dawa hizo.
Ripoti hiyo imeonesha kuwa watu milioni 35 duniani kote wanaishi na virusi vya HIV.(P.T)
Kulikuwa na maambukizi mapya milioni 2.1 mwaka 2013, asilimia 38 pungufu ya idadi ya milioni 3.4 mwaka 2001. Vifo vinavyotokana na UKIMWI vimepungua kwa humusi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, na kusalia katika milioni 1.5 kwa mwaka.
Afrika Kusini na Ethiopia zimeweza kupiga hatua kubwa. Sababu nyingi zinasaidia kubadili hali ilivyo, ikiwemo upatikanaji wa dawa. Kumekuwa na idadi mara dufu ya wanaume kutaka kufanya jando kama njia ya kupunguza hatari ya kupata au kusambaza virusi vya HIV.

CCM NA CHADEMA WAZICHAPA KAVUKAVU MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MAJI BW AMOSI MAKALA


 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana.

 Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika  akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla  akihutubia katika mkutano huo.

Poilisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada gani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.

Tuesday, July 15, 2014

CPC DODOMA KWA WAKA MOTO WANACHAMA WAWATUHUMU VIONGOZI KWA UBADHILIFU KATIBU AJIUZURU

Ofisa Mipango wa Umoja wa Club za waandishi wa Habari nchini [UTPC]Victor Maleko akiwa ameshika Box la Video Camera Mpya aina ya Canon Xa10 ambalo lilikuwa halina kitu na Camera hiyo kutojulikana ilipo kwenye ofisi ya waandishi wa habari Dodoma mara baada ya Mkutano mkuu maalum.

Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakishuhudia ukaguzi wa vifaa uliokuwa ukifanywa na wajumbe wa tume ya ufuatilaji iliyoundwa na mkutano mkuu maalum chini ya maofisa wa UTPC katika ofisi zao zilizopo katika ofisi za zamani za mkuu wa mkoa ambapo hata hivyo iligundulika kutokuwepo vifaa kadhaa bila kujulikana vilipo.

Aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma[CPC] Israel Mgusi akisoma tamko la kamati ya utendaji kujiuzuruambapo hata hivyo wanakamati wengine waliikataa kutokana na kubadili maamuzi yao na hivyo katibu huyo kujiuzuru pamoja na mjumbe Joel Mjengi.
Mkrugenzi wa umoja wa Club za waandishi wa habari Tanzania [ UTPC]Abubabari Karsan akifafanua mambo mbalimbali mbele ya wanachama wa Centrol Press Club [CPC] wakati wa mkutano mkuu maarumu wa wanahabari hao ulioshawishiwa na wanachama.
PICHA NA JOHN BANDA