Sunday, December 29, 2013

WATUMIAJI WA NYAMA YA KITI MOTO WAKO KWENYE HATARI YA KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIFAFA.


UTAFITI WA KISAYANSI uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo [SUA] umebaini walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wapo katika hatari ya kupata ugongwa wa kifafa kutokana na baadhi ya ngururuwe kuwa na minyoo inayopelekea ugonjwa huo. Hayo yalibainishwa na Mhadhiri n a Mtafiti wa Idara ya Sanyansi ya Wanyama na Uzalishaji SUA, Profesa Faustine Lekule alipokuwa akizungumza na mwandishi kutoka chombo cha serikali.

Profesa Lekule alisema, utafiti uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark [DANIDA] ulibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

Uchunguzi huo ulibaini kuwa, nyama hiyo kuwa na minyoo hatari iitwayo TEGU kuwa katika nyama hiyo, hivyo endapo kama nyama hiyo ikiliwa pasipo kuiva vizuri minyooo hiyo kawaida kukimbilia kichwani na hatima yake mlaji kukumbwa na tatizo la kifafa.

Alisema utafiti ulibaini baadhi ya wafugaji hawazingatiii kanuni za ufugaji na kuwaacha wanyama hao kujitafutia chakula wenyewe na wanyama hao kupelekea kula hata kinyesi cha binadamu, kutokana na wafugaji kujisaidia hovyo vichakani na ni moja ya sababu ya wanyama hao kupelekea kupata minyoo hiyo.

Hivyo binadamu nae anapokula nyama hiyo pasipo kuzingatia kanuni na kuila ikiwa haijaiva vizuri hadi minyoo hiyo kuisha ndani ya nyama hiyo hupelekea kupata madhara hayo kwa kuwa kuwa minyooo hiyo hukimbilia kichwani.

Alisema ugonjwa huo hautaweza kukwepeleka kwa walaji wa nyama hiyo kwa kuwa nyama nyingi husafirishwa na kusambazwa maeneo mengi na wanyama hao wengi hutokea maeneo ya mikoani mikoa mikubwa yenye mapori.

Profesa Lekule ameitaka serikali kwa ushirikiano wa wafugaji na wataalamu wa afya kushirikiana kwa hali na mali kudhibiti ugon jwa na kukabiliana na changamoto zilizopo kwakuwa,huo ambao ni hatari

No comments:

Post a Comment