Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza
maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai,
chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati
alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku
ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi
Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati alipotembelea
katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya
watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na
yeye kuzaliwa salama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment