Waimbaji wa nyimbo za injili watakaotumbuiza katika Tamasha la kusifu
[Shangwe za Xmas] Dodoma kutoka Nje ya nchi waendelea kuongezeka.
Ni Baada ya mwimbaji kutoka Nchini Kenya TUMSIFU RUFUTU mwimbaji wa
wimbo wa Mwambie Farao kuwa rasmi kwenye tamasha la Kristmas
litakalofanyika Dodoma Tar 25.12.2013 katika uwanja wa Jamhuri, Hatima
mwingine aongezeka kutoka nchini Somaria Bi. MARY SINKALA mwenye wimbo
wa Mkumbuke Muumba wako.
Tayali waimbaji hao wate wameshawataka wakazi wote wa mkoa huo na
vitongoji vyake na watakaotoka nje kujiandaa kwani wao wamejiandaa vya
kutosha na kwamba watawafundisha namna ya kumkumbuka muumba wao na
jinsi ya kuelekea kaanani.
Shangwe hizo ambazo kwa sasa ni gumzo mkoani humo kutokana na
kuandaliwa kwa umahili mkubwa na kampuni ya Liberty Promotion Company
ya mjini humo tayali wakurugenzi wake wamewataka watu kuhudhuri kwa
wingi kutokana na kiingilio kidogo kitakachomuwezesha kila mtu
kukimudu cha 2000 kwa wakubwa na watoto 1000.
Kampuni hiyo imesema Dodoma imekuwa nyuma kwa muda mrefu hasa nyakati
za Sikukuu za kidini na hivyo wamekusudia kukata kiu za wananchi
mkoani humo kwa shangwe za kumuimbia na kumtukuza mungu kupitia
matamasha ya mara kwa mara kuanzia na KRISTMAS ya mwaka huu, huku
wakiahidi kuibua vipaji vya chipukizi wengi.
Tamasha hilo litawaunganisha waimbaji toka ndani na nje ya nchi hasa
wa mikoa ya DSM na Dodoma itakayobebwa na waimbaji toka makanisa
mbalimbali na wachuo kikuu cha Dodoma [UDOM]
Mwimbaji wa nyimbo za injili
Toka nchini SomaliaMARY SINKALA
atakaeshiriki katika tamasha la kristmas litakalofanyika Dodoma Des 25
ndani ya uwanja wa jamhuri
atakaeshiriki katika tamasha la kristmas litakalofanyika Dodoma Des 25
ndani ya uwanja wa jamhuri
No comments:
Post a Comment