Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza bidhaa za ngozi Ndg. Shaban Lukandamila akimuonesha mkuu wa mkoa dodoma Dr Rehema Nchimbi bidhaa za ngozi zilizotengenezwa na vijana wajasiriamali wa manispaa ya Dodoma waliopatiwa mafunzo ya SIDO Dodoma ya utengenezaji bidhaa za ngozi. Mafunzo hayo yalifungwa jana na mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu wa mkoa dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi cheti kijana mjasiriamali SEIF DAUD aliyehitimu mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi kwenye kituo cha SIDO Dodoma kinachofundisha mafunzo hayo. Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa tatu kulia waliokaa) na vijana wajasiriamali 27 kutoka manispaa ya Dodoma waliopata mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi mara baada ya mkuu wa mkoa kufunga rasmi mafunzo hayo mapema jana kwenye kituo cha SIDO Dodoma kinachofundisha utengenezaji wa bidhaa za ngozi. Wengine waliokaa ni viongozi wa SIDO Dodoma na viongozi wa asasi ya marafiki wa elimu Dodoma waliofadhili mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment