LEO
imefahamika kwamba Dk Kitila amevuliwa madaraka hayo kwa muda
usiojulikana baada ya uongozi wa chuo hicho kupata taarifa kwenye vyombo
vya habari kuwa ni kiongozi wa Chadema huku akiwa mtumishi wa umma.
Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, ni kinyume cha sheria cha nchi mfanyakazi wa umma kuwa kiongozi katika chama cha siasa.
Kutokana na uamuzi wa chuo hicho wiki iliyopita Dk Kitila alipewa barua ya kusimamishwa.
Baada ya uamuzi huo Dk Kitila ataendelea kuwa mhadhiri mwandamizi kwenye kitivo hicho.
Hivi
karibuni Dk Kitila Mkumbo alivuliwa nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kushiriki kuandika
waraka wa badiliko ndani ya Chadema.
No comments:
Post a Comment