Na
John Banda,Dodoma.
IDARA
ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma imesema elimu inayotolewa na vyombo vya habari
kuhusu kuwafichua wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyemela bila kibali
halali.
Imefanikiwa
kutokana na mahusiano mazuri na Halmashari ambazo zimeamua kutekeleza kwa
kuziangiza ngazi zote za vijiji,kata hadi tarafa ziwe na kitabu cha
kuhodheresha wageni wote wanaoingia katika maeneo yao.
hayo
yamesemwa na Naibu Kamishana wa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Norah Masawe alipokuwa
akivishukuru vyombo vya habari, kwa kushirikiana katika utoaji wa taarifa ya
elimu inayotolewa na idara hiyo kwa taasisi,mashirika na wakazi wa mkoa huo.
Norah
alisema elimu hiyo inayotolewa kwa kupitia vyombo vya habari,aidha imeleta
mwitikio kwa watendaji wa ngazi zote za serikali na wananchi kuwa na utayari wa
kwenda mahakamani kutoa ushahidi tofauti na kipindi cha miaka ya nyuma.
Naibu
Kamishana huyo alisema kuwa hivi sasa elimu hiyo inayotolewa na Idara hiyo ya
Uhamiaji imeweza kuzifanya Halmashauri kuangiza watendaji wake kuwa na kitabu
cha kuandikisha wageni wanaoingia kwa lengo la kuwabaini wahamiaji haramu.
Alisema
hivi sasa watendaji kwa kushirikiana na wananchi wanashirikiana na Idara ya
Uhamiaji katika kuwabaini watu wanaoingia nchini kinyemela na kuamua kukaa
nchini huku wengine wakijishughulisha na kazi mbalimbali bila kibali halali.
“Unajua
hapo mwanzo utaratibu huu ulikuwepo kwa kila balozi wa nyumba kumi alikuwa na
kitabu cha kuhodheresha wageni wanaoingia katika maeneo yao na ndivyo
inavyotakiwa kwa hivi sasa kwa hali hiyo ili kuwabaini wahamiaji haramu”alisema
Norah.
Norah
alisema kuwa Mkoa wa Dodoma umekuwa na matukio mengi ya uingiaji wahamiaji
haramu na hatimaye kufanikisha kuwakamata,hii inatokana na wakazi hao kuwa na mahusiano
mazuri baada ya kupatiwa elimu ya jinsi ya kuwatambua wageni hao.
Aidha
Naibu huyo wa idara ya uhamiaji ameendelea kuwataka wananchi wa mkoa huo
kutoa ushirikiano katika kuwatambua wahamiaji hao haramu kwa kuwa watu hao
wanaishi kwenye maeneo yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment