Na John Banda, Dodoma
WATU watatu wanashikiliwa na polisi mkoani Dodoma kwa makosa ya utapeli kwa njia tofauti ikiwemo ya kutumia Dolla Bandia
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa hapa Suzan Kaganda alisema jeshi
hilo liliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Abuu Mohmed Omary maarufu
kwa jina la Rass Mfanya biashara soko la Sabasaba maeneo ya Nyerere
Squere.
Kaganda alisema Rass alikamatwa akijaribu kumrubuni Agostino
Mpanda alipokuwa akitaka kumtapeli 7, 500,000 kwa kutumia Dolla Bandia,
Dolla nyeusi [Black Dolla] ambapo huwaambia watapeliwa watoe fedha ili
kununulia Dawa ya kuzioshea.
Kaimu Kamanda huyo aliongeza kuwa baada ya kumkamata na
kumpekua mtuhumiwa huyo nyumbani kwake walimkuta akiwa na Shl 2,600,000
ambazo alishindwa kueleza namna alivyozipata.
Wakati huohuo
Jeshi hilo limewakamata Fransisika Gerard Mchaga mkazi wa Area E 27 na
Ibahimu Mkwawa Mhehe 40 mkazi wa ipagala wakiwa kwenye Gari aina ya NOAH
yenye namba za usajili T 311 BLM likitokea Morogoro kuja Dodoma.
Watu hao waliokamatiwa Wilaya ya Chamwino walikutwa na Chupa
kubwa ya Chuma yenye uzito wa kilo 15 ikiwa na lebo ya Red Mercury
Industry na Nembo ya UN iliyokuwa imejazwa Goroli ndogondogo za Baiskel
wanazodaiwa kutumia kwa Utapeli wakidai ni madini.
Jeshi hilo limewapongeza wananchi wanaolisaidia kufichua
waharifu na kuwataka kuendele ili hatimae waweze kupunguza kama siyo
kuondoa kabisa tatizo hilo la watu kujipatia Fedha kwa njia zisizo za
halali, huku jeshi hilo likiwataka wanaojihusisha na Utapeli wa namna
yoyote kuacha tabia hiyo kwani Sheria haitawafumbia macho.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment