Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz, akikwepa moja ya kopo la Bia lililorushwa na shabiki jukwaani hapo wakati
akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music
Tour, 'Kikwetu Kwetu', lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Dodoma, ikiwa ni shoo ya kwanza ya muendelezo wa Tour ya wasanii
walioshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards
2013, zilizomalizika hivi karibuni nchini.
Ommy, wakati akipanda jukwaani hapo aliuteka umati wa mashabiki walioripuka kumshangilia kwa makelele kibao, lakini alichafua
hali ya hewa pale aliposimama na kuanza kuzungumzia tukio lake
aliloripotiwa na moja ya gazeti sikun za hivi karibuni lililomripoti
kuwa alintusi marehemu Albert Mangwea.
Alianza kwa kusema, Jamani Naomba mnielewe mimi siwezi kumtukana Albert Mangwea, Yule ni Kaka yangu, na ninamheshimu sana
ila naamini nilishindwa kueleweka tu na kukaririwa tofauti, hata yeye
huko aliko anajua kuwa mimi sikumtukana na mungu anajua, nampenda sana
na ninamheshimu sana na pia nawapenda sana mashabiki.
Baada ya kumaliza kauli yake hiyo, alianza kuwarusha mashabiki kwa vibao vyake vinavyoeleweka na wengi huku wengine wakishangili,
na wengine wakitukana na kuzomea na pia wengine wakirusha makopo ya Bia
ya Castle jukwaani kumtwanga nayo wakimtaka kushuka jukwaani hapo,
jambo lililowafanya waandaaji kuwaamulu mabaunsa kumshusha jukwaani
ghafla na wacheza shoo wake na kuacha muziki wake ukiendelea kurindima
bila yeye jukwaani na baadaye kuzimwa na Dj, ambaye alikuwa hajafahamu
kinachoendelea.
Baada ya kushuka jukwaani Dimpoz, alisikika akijilaumu kwa kuelezea ukweli wake wa moyoni, huku akisema kuwa, ''Najua nimewaudhi
sana mashabiki wangu, lakini mimi nilikuwa naelezea ukweli wangu kutoka
moyoni, na sitaacha kueleza ukweli ili watu wanielewe kuwa mimi sikuwa
na nia ya kumtusi rafiki yangu, Kaka yangu, Marehemu Mangwea, Kiukweli
nilijisikia kuwaeleza ukweli mashabiki kwani niliona pale ndiyo
ningeweza kueleweka zaidi kutokana na umati mkubwa uliokuwapo eneo lile,
lakini nao pia walinipokea tofauti, ila naamini ipo siku nitaeleweka na
watu wataujua ukweli'', alisema Dimpoz
No comments:
Post a Comment