Marehemu, Jafari akiwa na mkewe Khadija Kopa, siku wa harusi yao mwaka 2008.
Habari
zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Kijana mtanashati
aliyekuwa Mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, aliyefahamika
kwa jina moja la Jafari, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali
ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akitibia kile
kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na kifua.
Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008.
Wakati
kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa
safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya
kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa
mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini.
Ratiba
kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa
huenda msiba huo ukawa maeneo ya Chaline au Lugoba ambako ni nyumbani
kwa wazazi wa Marehemu.
No comments:
Post a Comment