Saturday, June 15, 2013

MGOGORO KATI YA WAKULIMA WA NZUGUNI DODOMA NA CDA WAPAMBA MOTO WAZEE WA KIMILA WAAPA KUFANYA LOLOTE.



Kada wa Chama cha mapinduzi [CCM] Yared Jamal akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwatuliza wakulima ambao mashamba yao yanapimwa na CDA katika kijiji cha nzuguni Dodoma Bila wakulima hao kuwa na taarifa yoyote..



Mkuu wa Mambo ya kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akimwagilia maji juu ya mnara wa kumbukumbu wanaoujenga pembezoni mwa kisima cha maajabu Kilichopo katika mlima wa Bwibwi kijiji cha iyumbu Dodoma.



Polisi wakiingia kulinda usalama katika eneo  linalopimwa na CDA lililopo kijiji cha nzuguni manispaa ya Dodoma bila ya wakulima zaidi ya 100 waliokuwa wakilitumia eneo hilo kuwa na Taarifa yoyote.



Wafanyakazi wa Mamraka ya Ustawishaji makao makuu CDA wakipima eneo la wakulima lililopo kijiji cha nzuguni manispaa ya Dodoma huku kukiwa na mzozo kati yao.

upimaji ukiendelea kama kawaida.



                                [PICHA NA JOHN BANDA]

No comments:

Post a Comment