Washtakiwa 52 kati ya 54 katika kesi ya
kula njama na kufanya maandamano isivyo halali wamehukumiwa kwenda jela
kila mmoja baada ya kukutwa na makosa matatu huku mmoja akiachiwa huru
baada ya kukutwa hana hatia na mwingine kufariki dunia kabla ya hukumu
iliyotolewa leo na hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Hamimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda kosa Februari 15 mwaka huu.
Baada ya pande zote kusikilizwa na washtakiwa kutoa hoja za utetezi, hatimaye hakimu Fimbo alitoa hukumu hiyo leo ambapo aliwatia hatiani washtakiwa 52 kwa makosa matatu kati ya manne na kila mmoja akamhukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa kila kosa.
Hata hivyo, Fimbo akasema washtakiwa hao watakwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa vile adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.
Mshtakiwa aliyeachiwa huru baada ya kukutwa kuwa hana hatia ni Waziri Omari (namba 48), ambaye katika utetezi wake alidai kwamba siku ya tukio alikamatwa wakati akiwa katika shughuli zake za biashara ya kuuza kwa kutembeza barabarani vyombo vya nyumbani ikiwa ni pamoja na mabeseni.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo leo, wakili Mohamed Tibanyendera alimtaka hakimu awapunguzie adhabu wateja wake kwavile wengi wao wanategemewa na familia zao na kwamba, tayari walishakaa mahabusu kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.
Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Salum Makame, Said Idd na Ally Nandumbi, Makame, Idd na Nandumbi, Hussein Athumani, Seif Rwambo, Abdull Ally, Waziri Swed, Naziru Waziri, Ahmad Rashid, Jumanne Kayogola, Hamis Tita, Amri Diyaga, Salum Said, Rajabu Mpita na Haji Sheluhenda.
Wengine ni Abdul Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani Fadhili, Awadh Juma, Omari Mkwau, Kassim Chobo, Abubakari Bakari, Ramadhani Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah Salum, Juma Makoti, Bashir Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta na Bakari Athumani, Mbwana Kassim, Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma, Omari Mkandi, Idrisa Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu, Ramadhani Juma, Musa Sinde, Issa Sobo, Yahaya Salum, Jabil Twahil, Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri Toy, Athuman Yahaya, Yasin Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib Abdallah na Rajabu Rashid wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya tukio, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama za kufanya maandamano isivyo halali.
Shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha uvunjifu wa amani.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola, alidai katika shitaka la tatu kuwa siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, washtakiwa wote kwa pamoja baada ya Jeshi la Polisi kutoa zuio la kufanya maandamano, walikiuka amri hiyo na kufanya mkusanyiko ulisababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Katika shitaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.
VILIO, SIMANZI
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, vilio vilitawala katika viunga vya mahakama vilivyofurika watu kufuatia baadhi ya ndugu na jamaa wa washtakiwa kuangua kilio, wasiamini kile kinachotokea.
Baadaye washtakiwa walipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa gerezani

No comments:
Post a Comment