Sitaki tena uongozi... nimechoka kutukanwa...! -- Kaburu |
Simba tena basi... nawapisha wengine! -- Zacharia Hanspope |
Hali
ya mambo imezidi kuwa mbaya ndani ya klabu ya Simba baada ya Makamu
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Goefrey Nyange 'Kaburu' kuandika barua ya
kujizulu leo.
Hatua hiyo ya kubwaga manyanga kwa Kaburu, imekuja muda mfupi tu
baada ya kujiuzulu leo hii pia kwa mjumbe wa kamati ya utendaji ambaye
pia ni mwenyekiti wa kamati yao ya usajili, Zacharia Hanspope.
Kaburu amesema kwamba ameamua kubwaga manyanga kwa vile anaona kuwa
ni kazi ngumu kuongoza Simba kwani licha ya jitihada anazofanya katika
kushirkiana na wenzake ili waifikishe mbali klabu yao, bado amekuwa
akikumbana na matusi kila uchao na kuchoshwa na hali hiyo.
"Ni vigumu sana kuongoza klabu yetu. Viongozi tunatukanwa... sasa
nimechoka," amsema Kaburu, huku akiwatakia kheri wanachama wengine
watakaoongoza ili waifikishe mbali.
Hanspoppe amesema kuwa ameamua kujiuzulu kufuatia matokeo mabaya ya
timu yao katika mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara na pia kipigo cha
aibu walichopata katika michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika baada ya
kuchapwa kwa jumla ya mabao 5-0 na Recreativo de Libolo ya Angola.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, amekiri kupokea barua za kujiuzulu kwa Kaburu na Hanspope.
Wakati hayo yakitokea, mwenyekiti wa klabu hiyo inayoshikilia ubingwa
wa Tanzania Bara, Ismail Aden Rage, bado yuko nchini India alikokwenda
kwa matibabu.
Baadhi ya wanachama wa Simba wamekuwa
wakishinikiza viongozi wao kuachia ngazi kutokana na mfululizo wa
matokeo mabaya, lakini Rage aliwahi kupuuza rai ya kutakiwa kujiuzulu
kwa maelezo kwamba yeye siyo mchezaji wala kocha
No comments:
Post a Comment