Serikali
imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea
waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema
uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF
na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Amesema
baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato
huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya
wagombea walioenguliwa.
Rais
Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee,
pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu
kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali
ionekane imetendeka.
“Serikali
imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko
ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari.
Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano
tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze
kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.
Amesisitiza
kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na FIFA
baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF
hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya
maana hata kidogo.
Hivyo
amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi
na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza
wao na vyombo vilivyowaengua.
Pia
amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini
vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA
ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.
Amewakumbusha
wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina
katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.
Rais
Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za
wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano
ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa
No comments:
Post a Comment