Monday, July 3, 2017

MAJALIWA: CHANGAMOTO YA USAFIRI VIJIJINI KUWA HISTORIA

kuf1
,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akizindua  kitabu cha Muongozo  wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini ,katikati  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI .Simba  Chawene  ,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Wakala Barabara Vijini na Mijini Mhandisi  Victor Seif .Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017 katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
kuf2
,Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa. kulia   akimkabidhi kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini  , Mkurugenzi Mtendaji wa  Wakala Barabara Vijini na Mijini Mhandisi  Victor Seif, katikati  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI .Simba  Chawene  . Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017 katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
kuf3kuf4
Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akihutubia Viongozi wa Mikoa yote Nchini walio hudhuria  Uzinduzi  wa Wakala  wa Barabara Vijini na Mijini leo july 2,2017, katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma.
kuf5kuf6
Wakuu wa Mikoa na viongozi mbalimbali wakishuhudia   Uzinduzi wa Wawakala wa Barabara Vijijni na Mijini
 Picha na ofisi ya Waziri Mkuu
…………………………………………………………….
               *Azindua Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini 
                *Asema utashusha bei ya vyakula mijini
 CHANGAMOTO ya usafiri nchini, hususan maeneo ya vijijini kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
 Amesema wakala huo utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo kukuza uchumi.
 Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili,  Julai 02, 2017) wakati akizindua wakala huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.
 “Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa na manufaa makubwa kwa ustawi wa nchi yetu kwa kuongeza chachu ya uzalishaji mali mashambani kutokana na urahisi wa kufika sokoni,”
 “Utashusha bei ya vyakula mijini na bidhaa za viwandani vijijini kutokana na gharama za usafirishaji wa mazao kutoka mashambani na bidhaa za viwandani kutoka mijini kupungua,”
 Aidha, Waziri Mkuu amesema manufaa mengine ya wakala huo ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na kiuchumi kwa wananchi kwani watakuwa wanasafiri kwa muda mfupi.
 Pia utawezesha maeneo mengi ya nchi kufikika kwa urahisi, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wakati.
 Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika ujenzi, ukarabati na utengenezaji wa miundombinu ya barabara ikiwemo ya rushwa katika utoaji wa zabuni.
 Amesema jambo hilo halikubaliki hivyo, amewataka watendaji wa TARURA wahakikishe wanatokomeza vitendo vya rushwa vilivyokithiri kwenye utoaji wa zabuni, zitolewe kwa watu wenye uwezo wa kufanyakazi.
 Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine ni usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi, ambapo ameelekeza isimamiwe vizuri na iwe ya wazi na yenye kutekelezeka.
 Akizungumzia vitendo vya baadhi ya viongozi wa Halmashauri kubadilisha matumizi fedha za barabara, ameagiza fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya barabara zitumike kama ilivyopangwa.
 Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa George Simbachawene alisema TARURA ni muhimu kwa kuwa zinagusa wananchi moja kwa moja na ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa wananchi, hivyo kuinua uchumi wa  Taifa wenye msingi imara.
 “Barabara hizi zinachochea kilimo katika ngazi ya jamii, zinaboresha ufikaji kwenye huduma za kijamii kama afya, elimu, maji na masoko, hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na jamii imara kiafya, kiakili na kiuchumi,”.
 Kutokana na umuhimu wa mtandao wa barabara za Vijijini na Mijini, Mheshimiwa Simbachawene ameomba mgawanyo wa mapato ya Mfuko wa Barabara wa asilimia 70 kwa TANROADS  na asilimia 30 kwa Halmashauri uangaliwe upya, ambapo Waziri Mkuu ameridhia.
 Waziri Mkuu alisema “Naamini kwa kuanzishwa TARURA sasa hoja hii inajadilika, tumieni taratibu zilizopo ili maamuzi yaweze kufanyika,”.
Mtandao wa barabara za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kilomita 108,942.2 ambao ni Zaidi ya nusu ya barabara za Kitaifa.

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KALI KWA WANASIASA WANAOSHABIKIA MAOVU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Joseph Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotaka sifa za kisiasa kwa kushabikia waovu hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Rais amesema kuna watu wanashabikia maovu kwa kutoa matamko bila kuyapima madhara yake.
“Niwaombe wanasiasa wanaoshindwa kuzuia midomo yao, wanaosema kuwa hawa watu wameshikiliwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu, katika hali hiyo kwanini usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.
Msitufanye tukafika huko,” Rais John Magufuli. “Kwanini hata siku moja mtu asijitokeze kulaani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa kuta sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule…nataka polisi mfanye kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani,” amesema Rais John Magufuli
“Juzi mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa waliogiza hizo uniform za jeshi,” Rais John Magufuli.
“Endeleeni kujenga heshima ya bandari, rushwa iwe ni marufuku, halafu muda pia… mtu akifika hapa akae muda mfupi na aondoke, hata kama anasafirisha pini ifike inapokwenda na sio ipotelee njiani,”
Rais John Magufuli “Kuna vichwa 13 vya treni vimeshushwa hapa lakini havijulikani ni vya nani, tena inasemekana ni vibovu na TRL wamesema hawajaagiza na wala hawajasaini mkataba wowote.
Hamkuuliza vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku nyingine si watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu,” Rais John Magufuli “Sijui haya mavichwa mtafayanyia nini, lakini hili ni lazima lisemwe ili Watanzania wafahamu. Tutangulize uzalendo wa nchi yetu.

BAADHI YA WAKURUGENZI WA MANISPAA MBALIMBALI WASHIRIKI UZINDUZI WAKALA WA BARABARA MIJINI NA VIJIJINI (TARURA) MJINI DODOMA.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Ndg John Lipesi Kayombo ameungana na wakurugenzi wengini nchini kuhudhuria Mkutano wa Uzinduzi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini uliofanyika Kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo katika Chuo Cha Mipango Mjini Dodoma Leo Julai 2, 2017.
Mkurugenzi Kayombo ameshiriki Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (MB) wenye dhamira ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya Barabara nchini kutokana na kuanzishwa kwa wakala wa barabara Mijini na Vijijini.
Uanzishwaji wa Wakala wa Barabara nchini ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015 iliyopo katika ukurasa wa 54 inayoielekeza serikali kuanzisha Wakala/Taasisi itakayosimamia kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za Halmashauri, Miji, na Majiji ambazo zipo chini ya TAMISEMI ifikapo mwaka 2020.
Katika Mkutano huo zimeelezwa changamoto mbalimbali zinazozikabili mamlaka za serikali za Mitaa katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya Barabara ambazo ni pamoja na Miradi kutekelezwa kwa viwango duni, Ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi kutokana na mipango isiyoridhisha, Kandarasi kutolewa bila kuzingatia vigezo, uwezo na sifa.
Changamoto zingine ni pamoja na kutokuwepo kwa viwango vinavyoshabihiana vya ubora wa barabara Kati ya Halmashauri Moja na nyingine, Fedha zilizopangwa kutekeleza miradi ya barabara kutotumika kutokana na urasimu wa viongozi wa Halmashauti, Rushwa iliyokithiri katika utoaji wa zabuni, Mgongano wa maslahi na usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi.
Wakala huu utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na hivyo kuwawesesha wananchi wengi zaidi kusafiri na kusafirisha bidhaa za mashambani kwa urahisi.
Katika Mkutano huo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Majaliwa K. Majaliwa akizungumza kabla ya kuzindua Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini alieleza manufaa yatakayopatikana kutokana na kuwa na Barabara za Vijijini na Mijini kuwa ni pamoja na kuongeza chachu ya uzalishaji Mali mashambani kutokana na urahisi wa kufikisha mazao sokoni, Kushusha bei ya vyakula mijini kutokana na gharama za kusafirisha mazao kutoka mashambani kupungua.
Mengine ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na kiuchumi kwa wananchi, kufanya maeneo mengi zaidi ya nchi kufikika kwa urahisi na hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na Kutoa ajira kwa vijana katika maeneo ambayo ujenzi au ukarabati wa miundombinu utakapokuwa unafanyika.
Katika Mkutano huo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, imewakilishwa na Mkurugenzi Kayombo ambaye ameambatana na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Zimamoto Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga.

MSEMAJI WA POLISI ATUMBULIWA.

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amemteua Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa kuwa msemaji mpya wa jeshi hilo, akichukua nafasi ya Kamishina Msaidizi, Advera John Bulimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Uteuzi wa Mwakalukwa unatajwa kuwa moja ya harakati za IGP Siro kulifanyia mabadiliko jeshi hilo, katika kuboresha utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kujizatiti na mapambano ya uhalifu.
Kabla ya uteuzi huo, Kamishina Msaidizi Mwakalukwa amelitumikia Jeshi la Polisi kwa nafasi na nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kamanda wa Oparesheni wa mikoa mbalimbali pamoja na ngazi zingine za utumishi wa juu

Thursday, June 8, 2017

MATUKIO:PICHA MBALIMBALI UWASILISHWAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/2017

Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwaonyesha waandishi wa Habari mkoba wenye hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.
 Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18.
 Wabunge wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 Baadhi ya wageni wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 .Wabunge wakiingia Ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.

Picha zote na MAELEZO, DODOMA

Tuesday, June 6, 2017

RAIS JOHN POMBE MAGHUFULI AMWAPISHA RASMI ANNA ELISHA MGHWIRA KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO.


unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akisaini Hati ya Kiapo cha Udilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wengine Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi pamoja na wakuuu wa Wilaya za Ubungo na Ilala wakipiga makofi
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akielekea kwenye gari tayari kabisa kwa kuondoka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
3
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akiwa amekaa kabla ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MH WAZIRI MKUU KHASIMU MAJALIWA AZINDUA ZOEZI LA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA MAABARA NCHINI

unnamed
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la  usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
1
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akipata maelekezo toka kwa moja ya mwalimu wa masomo ya sayansi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
2
 Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
3
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhi moja ya kifaa cha kufundishia masomo ya sayansi kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Juhudi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
4
 Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
5
Baadhi ya wanafunzi  wa shule za Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo