Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Joseph Pombe Magufuli
ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotaka sifa za kisiasa kwa kushabikia
waovu hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam
Rais amesema kuna watu wanashabikia maovu kwa kutoa matamko bila
kuyapima madhara yake.
“Niwaombe wanasiasa wanaoshindwa kuzuia midomo yao, wanaosema kuwa
hawa watu wameshikiliwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu
kule Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu, katika hali hiyo kwanini
usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.
Msitufanye tukafika huko,” Rais John Magufuli. “Kwanini hata siku
moja mtu asijitokeze kulaani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa
kuta sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda
mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule…nataka polisi mfanye kazi yenu,
hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa
haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa
kule ndani,” amesema Rais John Magufuli
“Juzi mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika
na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni
miongoni mwa waliogiza hizo uniform za jeshi,” Rais John Magufuli.
“Endeleeni kujenga heshima ya bandari, rushwa iwe ni marufuku, halafu
muda pia… mtu akifika hapa akae muda mfupi na aondoke, hata kama
anasafirisha pini ifike inapokwenda na sio ipotelee njiani,”
Rais John Magufuli “Kuna vichwa 13 vya treni vimeshushwa hapa lakini
havijulikani ni vya nani, tena inasemekana ni vibovu na TRL wamesema
hawajaagiza na wala hawajasaini mkataba wowote.
Hamkuuliza vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku
nyingine si watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu,” Rais
John Magufuli “Sijui haya mavichwa mtafayanyia nini, lakini hili ni
lazima lisemwe ili Watanzania wafahamu. Tutangulize uzalendo wa nchi
yetu.
No comments:
Post a Comment