,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua
kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
,katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI .Simba Chawene
,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara Vijini na Mijini
Mhandisi Victor Seif .Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017 katika
ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kulia
akimkabidhi kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini na
Mijini , Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara Vijini na Mijini
Mhandisi Victor Seif, katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI .Simba Chawene . Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017
katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akihutubia Viongozi wa Mikoa yote Nchini walio hudhuria Uzinduzi wa
Wakala wa Barabara Vijini na Mijini leo july 2,2017, katika ukumbi wa
mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma.
Wakuu wa Mikoa na viongozi mbalimbali wakishuhudia Uzinduzi wa Wawakala wa Barabara Vijijni na Mijini
Picha na ofisi ya Waziri Mkuu
…………………………………………………………….
*Azindua Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
*Asema utashusha bei ya vyakula mijini
CHANGAMOTO ya usafiri nchini, hususan
maeneo ya vijijini kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kuzindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Amesema wakala huo utasaidia kuimarisha
mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi kusafiri
na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo kukuza uchumi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumapili, Julai 02, 2017) wakati akizindua wakala huo katika ukumbi wa
Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.
“Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa na
manufaa makubwa kwa ustawi wa nchi yetu kwa kuongeza chachu ya
uzalishaji mali mashambani kutokana na urahisi wa kufika sokoni,”
“Utashusha bei ya vyakula mijini na
bidhaa za viwandani vijijini kutokana na gharama za usafirishaji wa
mazao kutoka mashambani na bidhaa za viwandani kutoka mijini kupungua,”
Aidha, Waziri Mkuu amesema manufaa
mengine ya wakala huo ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na
kiuchumi kwa wananchi kwani watakuwa wanasafiri kwa muda mfupi.
Pia utawezesha maeneo mengi ya nchi kufikika kwa urahisi, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto
mbalimbali katika ujenzi, ukarabati na utengenezaji wa miundombinu ya
barabara ikiwemo ya rushwa katika utoaji wa zabuni.
Amesema jambo hilo halikubaliki hivyo,
amewataka watendaji wa TARURA wahakikishe wanatokomeza vitendo vya
rushwa vilivyokithiri kwenye utoaji wa zabuni, zitolewe kwa watu wenye
uwezo wa kufanyakazi.
Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine
ni usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi, ambapo ameelekeza isimamiwe
vizuri na iwe ya wazi na yenye kutekelezeka.
Akizungumzia vitendo vya baadhi ya
viongozi wa Halmashauri kubadilisha matumizi fedha za barabara, ameagiza
fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya barabara zitumike kama
ilivyopangwa.
Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa George Simbachawene alisema TARURA ni muhimu
kwa kuwa zinagusa wananchi moja kwa moja na ni kichocheo kikubwa cha
uchumi wa wananchi, hivyo kuinua uchumi wa Taifa wenye msingi imara.
“Barabara hizi zinachochea kilimo
katika ngazi ya jamii, zinaboresha ufikaji kwenye huduma za kijamii kama
afya, elimu, maji na masoko, hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na jamii
imara kiafya, kiakili na kiuchumi,”.
Kutokana na umuhimu wa mtandao wa
barabara za Vijijini na Mijini, Mheshimiwa Simbachawene ameomba mgawanyo
wa mapato ya Mfuko wa Barabara wa asilimia 70 kwa TANROADS na asilimia
30 kwa Halmashauri uangaliwe upya, ambapo Waziri Mkuu ameridhia.
Waziri Mkuu alisema “Naamini kwa
kuanzishwa TARURA sasa hoja hii inajadilika, tumieni taratibu zilizopo
ili maamuzi yaweze kufanyika,”.
Mtandao wa barabara za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kilomita 108,942.2 ambao ni Zaidi ya nusu ya barabara za Kitaifa.
titanium price per ounce - TIPS TIPS TIPS
ReplyDeleteAll titanium white octane Tinti gold Tinti is crafted in chi titanium flat iron titanium metal, it has a heat 출장마사지 index of citizen titanium dive watch 2500 to 5000 and is a true platinum-quality gold trekz titanium pairing alloy.