Mama FATMA KARUME akivishwa nishani ya heshima kwa niaba ya hayati ABEID AMAN KARUBE.
Rais mstaafu wa tanzania wa awamu ya nne MH JAKAYA KIKWETE akivishwa nishani ya heshima na makamu wa rais MH SAMIA SULUHU.
Rais mstaafu wa zanzibar akivishwa nishani.
Rais mstaaf wa awamu ya pili MH ALLY HASSAN MWINYI akivishwa nishani ya heshima na makamu wa rais MH SAMIA SULUHU.
Makamu wa rais MH SAMIA SULUHU akimvisha nishani ya heshima waziri mkuu staafu MH SALIMU AHMED SALIMU katika maadhimisho ya miaka 100 ya SCAUT TANZANIA.
Makamu wa rais mh SAMIA SULUHU HASAN akiongea katika maadhimisho ya miaka 100 ya SCAUT mjini dodoma.
Wednesday, July 26, 2017
Thursday, July 20, 2017
RAIS WA BURUNDI MH:PIERRE NKURUNZINZA AFANYA ZIARA YA SIKU MOJA TANZANIA.
Rais
wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara
kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini
Ngara 20 Julai 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais
wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara
uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai
2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea
Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika
viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 2017
Rais
wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwapungia wananchi
alipowasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai
20,2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa
Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwa wamesimama wakipokea salamu za
heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama.
Rais
wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akikagua graride la lililoandaliwa na
jeshi la ulinzi la Tanzania JWTZ katika viwanja vya Lemela mjini Ngara
Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Kumpokea
katika Uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa
Ngara kwenye uwanja wa Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta
Jambo na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza Mara baada ya kumpokea
katika Mji wa Ngara kwenye uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera
20 Julai 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza kwa
maongezi mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
ujumbe wake katika mazungumzo maalum ya kiserikali na Rais wa Burundi
Mhe. Pierre Nkurunziza na ujumbe wake Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai
2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa
Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza pamoja na mama Janeth Magufuli katika
Maongezi.
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono
wananchimwa mji wa ngara wakati wakiwasili katika uwanja wa posta mjini
Ngara kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono
wananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini
Ngara kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Umati
wa ananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini
Ngara kusikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli katika uwanja wa posta mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza katika uwanja wa
Lemela Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017 baada ya kumaliza ziara
yake Rasmi ya kiserikali Nchini. PICHA NA IKULU.
Wednesday, July 19, 2017
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa
uzinduzi wa Ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa
afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM). (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionyesha kitabu chenye
ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika
kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM) mara baada ya kuzindua taarifa
hiyo kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan leo amezindua Taarifa ya Nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za
Umoja wa Afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM).Uzinduzi huo
ulihudhuriwa na kiongozi wa Jopo la Mchakato huo kwa Tanzania ambaye
pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Watu Mashuhuri Bi. Brigitte Sylvia
Mabandla, Viongozi wengine wa APRM Tanzania ni Balozi Ombeni Sefue,
Profesa Hasa Mlawa na Balozi Aziz Mlima aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Mawaziri
wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
APRM
ni mpango wa hiari wa kujipima kwa vigezo vya utawala bora uliobuniwa
mwaka 2003 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa
Afrika. Lengo la mpango huu ni kuziwezesha nchi wanachama kujitathmini
kwa vigezo vya utawala bora katika maeneo manne ambayo ni; Demokrasia na
Utawala wa Kisiasa; Usimamizi wa Uchumi; Utendaji wa Mashirika ya
Biashara; na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.
Akihutubia
katika uzinduzi huo, Makamu Rais amewapongeza Wakuu wa Nchi na Serikali
wanaoshiriki katika mchakato wa APRM kwa ujasiri wao wa kushirikishana
taarifa za kuaminika kuhusu masuala ya utawala bora katika nchi zao.
“Taarifa hizi zinaonesha wazi juu ya hali ya utawala bora katika Bara
letu na kutupa nafasi ya kujirekebisha pale ambapo kuna dosari na
kujipongeza pale tunapofanya vizuri na kuwapa wengine nafasi ya
kujifunza zaidi’’ alisema Makamu wa Rais.
Aidha
alisisitiza kuwa kupitia utaratibu huu tumeweza kuuonesha ulimwengu
nguvu zetu za pamoja kama Bara la Afrika katika kuboresha demokrasia,
amani na utulivu, utawala wa sheria na utawala bora kwa ujumla.
Kwa
upande wa Tanzania, Makamu wa Rais alisema mchakato huu unatuonesha na
kutukumbusha falsafa na maono ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere
(Tujisahihishe, 1962) na Mwongozo wa TANU wa mwaka 1971. Alisema nchi
yetu imefanya mambo mengi katika kutekeleza mpango huo ikiwemo
kuimarisha taasisi zinazoshughulikia masuala ya utawala bora ikiwemo
Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora, taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.
Kuhusu
changamoto zilizobainishwa kwenye taarifa husika, Makamu wa Rais
alisema kwa kiasi kikubwa zimepatiwa ufumbuzi katika Mkakati wetu wa
Maendeleo 2025 unaolenga kukuza na kupanua wigo wetu wa uchumi ili kuwa
nchi ya uchumi wa viwanda. Kuhusu suala la Muungano alisema muundo wa
Muungano wetu ni wa serikali mbili ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu
wa Rais alisema miongoni mwa maeneo ya vipaumbele katika mchakato wa
kuelekea kuwa nchi ya viwanda ni kuimarisha sekta ya nishati na umeme.
“Kwa ujumla tumefanya jitihada kubwa katika huduma ya nishati kutokana
na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia hapa nchini” alisisitiza Makamu wa
Rais. Kwa sasa umeme unasambazwa kwa kasi katika vijiji vyetu kupitia
Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Serikali
imefanya jitihada kubwa katika kuzipatia ufumbuzi changamo za kijamii
kama vile elimu, afya na maji ambazo zilitajwa kama vikwazo katika
taarifa husika. Aidha, Serikali imeongeza uandikishaji wa wanafunzi kwa
shule za msingi na sekondari, imeboresha mazingira ya kujifunzia na
kufundishia, imejenga madarasa na maabara, imeboresha maslahi ya walimu
na kuhakikisha inajenga vyuo vya ufundi katika kila wilaya.
Pia
Makamu wa Rais alisema Tanzania inatambua kuwa mchakato huu wa APRM ni
endelevu hivyo serikali itaendelea na jitihada zake kuhakikisha kwamba
changamoto zote zilizobainishwa ndani ya taarifa zinapatiwa majawabu
kupitia serikali na taasisi zake, asasi binafsi na wananchi kwa ujumla.
Mwisho,
alishukuru na kutambua mchango wa washirika wa maendeleo katika
kufadhili kazi za APRM na kuwaalika kuendelea kuchangia shughuli za
APRMTanzania ikiwemo mpango kazi wa Taifa.
Tuesday, July 18, 2017
IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO JESHI LA POLISI.
Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ndani ya jeshi hilo.
Katika
mabadiliko hayo, Kamanda Sirro amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi
mkoa wa kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao
na Fidia Makao Makuu ya Polisi.
Taarifa iliyotolewa
leo Jumanne, Julai 18 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnaba Mwakalukwa,
imeeleza kuwa nafasi ya Kaganda imechukuliwa na Kamishna Murilo
Jumanne.
Kabla ya hapo, Kamanda Jumanne alikuwa Kamanda wa Polisi, mkoa wa Shinyanga.
“Nafasi
iliyokuwa ikishikiliwa na Jumanne, Shinyanga, imechukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa Polisi, (ACP) Simon Sylverius ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu
wa Polisi Mkoa wa Mara,” amesema.
Taarifa hiyo imesema,
mabadiliko hayo ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi ili
kuongeza ufanisi na utendaji wa kazi.
MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAMIA KUMUAGA LINAH MWAKYEMBE JIJINI DAR ES SALAAM.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hasan amewaongoza waombolezaji kuuaga mwili
wa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo marehemu Linah
George Mwakyembe katika usharika wa kanisa la KKKT- Kunduchi DSM.
Pamoja
na Makamu wa Rais, pia ibada hiyo imehudhuriwa na marais wastaafu mzee,
Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete pamoja na Mawaziri, Katibu Mkuu
kiongozi, makatibu wakuu na wawakilishi kutoka ofisi ya Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.
Akizungumza mmoja ya watoto wa Waziri
Mwakyembe ambaye amesoma wosia wa marehemu mama yake, Bi Linah amesema
mama yake alikuwa ana ngozi ngumu kuliko hata mzee wake na alikuwa
akimfariji na kumpa moyo endapo zinapotokea changamoto katika kazi yake.
Waziri wa Habari Dkt Harrison
Mwakyembe akilia kwa uchungu juu ya Jeneza la mkewe wake Linah Mwakyembe
wakati wa kutoa heshima za mwisho leo.
Marehemu Linah Mwakyembe mzaliwa wa
Machame Wari huko Kilmanjaro mwaka 1970 na alifariki dunia tarehe Julai
15 mwaka huu saa tano usiku katika hospitali ya AGA KHAN alipokuwa
anauguzwa maradhi ya saratani ya matiti ambayo imemsumbua kwa miaka
miwili na ameacha mume na watoto watatu wa kiume.
Sunday, July 16, 2017
PICHA MBALIMBALI ZA MH RAIS MAGUFULI AKIWA KANISANI CHATO KATIKA IBADA YA JUMAPILI.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na mke wake MamaJaneth
Magufuli wakitoa sadaka wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la
Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai
2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakisikiliza mahubiri toka kwa
Padri Henry Mulinganisa wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la
Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai
2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo wakati wa
ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia ya
Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka
akipokea sadaka toka kwa Mke wake Bi Janeth Magufuli wakati wa kuchangia
ujenzi na upanuzi wa katika kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia
ya Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka
akipokea sadaka toka kwa waumini mbalimbali waliohudhuria ibada katika
kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita Leo 16
julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa ameshika kikapu chenye
michango ya fedha zilizotolewa na waumini wa kanisa Katoliki la Bikira
MariaParokia ya Chato Mkoani Geita kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa
kanisa hiloLeo 16 julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru mmoja wa waumini wa
kanisa hilo ndugu Mwita Chacha mara baada ya kuchangia mifuko mitano ya
saruji kwaaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira
MariaParokia ya Chato Mkoani Geita .
Mama Janeth Magufuli mke wa Rais
wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiahidi
mchango wake wa ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira
MariaParokia ya Chato Mkoani Geita .
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akishuhudia mmoja wa waumini wa
kanisa hilo ndugu Deogratius Ambrosi mwenye ulemavu wa mkono,akitoa
mchango wake wa kiasi cha shilingi elfu tano kwaajili ya ujenzi na
upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani
Geita
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru mmoja wa waumini wa
kanisa hilo ndugu Deogratius Ambrosi mwenye ulemavu wa mkono,akitoa
mchango wake wa kiasi cha shilingi elfu tano kwaajili ya ujenzi na
upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani
Geita
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiondoka kwenye kanisa
Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita, mara baada ya
ibada.
Waumini wa kanisa Katoliki la
Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita wakimpungia mikono Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakati akiondoka
kanisani hapo.
Katibu wa Rais Ndugu Ngusa Samike
akikabidhi mchango wa Mhe Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Joseph Magufuli jumla ya shilingi milioni kumi kwaajili ya
ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato
Mkoani Geita,
Waumini wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita wakiwa kwenye ibada
Waumini wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita wakitoka kwenye ibada ya jumapili. (PICHA NA IKULU)
Subscribe to:
Posts (Atom)