Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu
juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga
hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye
hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi
ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda
kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro,
Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo
imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi,
Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika
ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika picha kulia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa
wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates
muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders
Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu
saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount
Meru jijini Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment