Makamu
Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya
(katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa
habari Maelezo.
Na Thehabari.com
KAMATI ya
Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja
na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya
utangazaji.
Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.
Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta
kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua
zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema
vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni
kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM
kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la
Ng'ombe.
Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.
Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa
kufanya.

Kamati
Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni
Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi
ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.
Hata hivyo
mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa
waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo
waandishi kubaki wameduwaa
wakiviamini vituo hivyo.
No comments:
Post a Comment