Habari
zilizoufikia mTANDAO HUU hivi punde kutoka Jijini Arusha zinaTAarifu
kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Ask Thomas Laizer,
PICHANI amefariki dunia.
Imeelezwa kuwa Askofu. Laizer amefikwa na umauti alasiri ya jana katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya jijini Arusha.
Februari
6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea na kumjulia hali
Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Taarifa
zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya
mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa
unaomsibu.
Pinda
alikwenda hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu
saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa
cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Hata
hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi
kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari
na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa
kuzungumza naye.
Awali
ilisemekana kuwa Askofu Laizer amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa
ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika
Selian kutaka kumwona, lakini jana ilidhihirika kuwa, amelazwa
hospitalini hapo.
FK
Blog inatoa pole kwa Waumini na washarika wote wa KKKT nchini kote
kufuatia msiba huo mzito ulilolikumba Kanisa la Kilutheri hasa wakati
huu ambao kuna mgongano kati ya waumini na Viongozi wa Dayosisi ya
Kaskazini Kati.
No comments:
Post a Comment