Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji
wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo,
zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara
wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha
dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya
maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani
alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) la
kujadili tafiti z\ilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha
zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri
26 nchini.
Meneja
wa Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa
(MSD), Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha
huduma nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu
matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya
katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa
wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi
ikiwemo Cameroon.
Msajili
wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati
ya usajili wa maduka ya dawa baridi vijijini wakati wa kongamano hilo
No comments:
Post a Comment