Wednesday, February 27, 2013

RUNGU LA TCRA LAIKUMBA CLOUDS FM KIPINDI CHAO CHA PIGWA STOP


Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo.
Na Thehabari.com
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na  Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa
kufanya.
Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.
Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa

*MSD YAWEKA WAZI WANAOWALINDA WANAOTOROSHA DAWA NJE YA NCHI



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti z\ilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini.
 Meneja wa Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD),  Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi ikiwemo Cameroon.
Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati ya usajili wa maduka ya dawa  baridi vijijini wakati wa kongamano hilo

Friday, February 22, 2013

OFISA MAENDELEO WA FIFA Ashford Mamelodi KUKTANA NA WANAHABARI TFF KESHO


Waandishi wa habari za michezo mnatangaziwa kuwa, Ofisa Maendeleo wa FIFA Kusini mwa Afrika, Ashford Mamelodi, atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika kesho Jumamosi (Februari 23 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF saa 5 kamili asubuhi. Tafadhali zingatia muda

KARIBU RAIS MWAI KIBAKI.

 Vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini akiagana na Makamu wa Rais Dkt Mohammed Ghalib Bilali aliye pamoja na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini wakisimama kupokea heshima wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam

Tuesday, February 19, 2013

MKUU WA KANISA LA OTHODOX ALIPOWASILI TANZANIA

8E9U1555Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II(wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Askofu wa Mwanza na Bukoba Askofu Jeronymos. Nyuma ya Rais mwenye tai nyekundu ni mwenyekiti wa Hellenic society of Tanganyika Dimitris Mantheakis,  na kulia ni askofu mkuu wa Dar es Salaam na mashariki askofu Dimistrious.(picha na Freddy Maro)

mh.lowassa akabidhi bajaji

bajaji1 1940c
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mh Edward Lowassa amekabidhi pikipiki  nne za miguu mitatu maarufu kama majaji za kubebea mizigo  zenye thamani ya kiasi cha  shilingi millioni 50 kwa umoja wa vijana wilaya ya Monduli, ili kusaidia vijana kukabiliana na tatizo la Ajira.Pichani Mh Lowassa akikabidhi pikipiki hizo kwa mmoja wa viongozi wa matawi ya vijana wilayani hapo, yumbani kwake Ngarash Monduli.

mwanafunzi ajiua kwa kujichoma moto

MSIBA WA MOTO 2 879d6

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Nzuguni iliyopo manispaa ya Dodoma amekufa kwa kujichoma moto baada ya Mjomba wake kumchapa viboko kutokana na kosa la kutomsaidia Bibi yake kuosha vyombo.

Tukio la kifo cha mwanafunzi huyo lilitokea jana jumapili ambapo saa 11 jioni katika hospital Rufaa ya General Dodoma baada ya kulazwa kwa masaa kadhaa

Wednesday, February 13, 2013

CHOMBO KIPYA CHA TAIFA STARS KUTOKA TBL



KIOTA KIPYA CHA DISCO NDANI YA ARUSHA

 Jengo la World Garden maeneo ya Mushoni jijini Arusha 
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Magesa Mulugo akiwasili eneo la jengo la World  Garden ili  jengo hilo  ambalo lina kumbi za mikutano pamoja na
ukumbi mkubwa wa Disco ambapo inadaiwa kwa uapande wa Afrika mashariki na kati hamna jengo kama hilo 
 Kwa ubavun

REAL MADRID NA MAN U HAKUNA MBABE ZATOKA SARE YA 1-1

 Mshambuliaji wa timu ya Manchester United, Danny Welbeck (kulia) akiruka kupiga kichwa na kuifungia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza, dhidi ya Real Madrid, wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa, uliochezwa usiku huu. Hadi zinamalizika dakika 90, timu hizo zimetoka sare ya 1-1, ambapo bao la Madridi la kusawazisha limefungwa na Christian Ronaldo.
Christian Ronaldo, akishangilia bao lake aliloisawazishia timu yake katika kipindi cha kwanza

YANGA NOMA KWELIIIIIIIII YAUA 4-0 NESHINO

 Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa African Lyon, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-0, mabao 2, yakifungwa na Jerry Tegete, bao la 3 limefungwa na Didier Kavumbagu na bao la 4, limefungwa na Nizar Khalfan.
 Pande la maudhi, Haruna Niyonzima (katikati) akitoa pasi ya maudhi huku huku akiwa katikati ya wachezaji wa African Lyon.

Tuesday, February 12, 2013

*CCM YATEUA MAJINA YA WAJUMBE 14 WA KAMATI KUU CCM TAIFA MJINI DODOMA


Mwenyekiti-wa-CCM-Taifa-Rais-Jakaya-Kikwete.

Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kilichofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili kuanzia 
Februari 10 na 11, 2013, pamoja na kuzungumzia mambo mengine kimeridhia kufanya uteuzi na kufanya uchaguzi wa 
Wajumbe 14 wa Kamati Kuu ya CCM.

Katika Kikao hicho Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia kuteuliwa kwa Dkt. Salim Ahmed Salim, ambaye 
ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Dkt.  Jakaya Mrisho 
Kikwete.

Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-
WAJUMBE WA KAMATI KUU TANZANIA BARA.
1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira
WAJUMBE WA KAMATI KUU-ZANZIBAR.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud

VITA YA WAISLAM NA WAKRISTU GEITA YAFIKIA PABAYA, MCHUNGAJI ACHINJWA HADI KUUAWA



Machafuko makubwa yametokea   katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa ni waumini  wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.

Habari za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.

Imeelezwa kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya waislamu.

Tukio hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la kuifunga.

Wakati wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa maandishi BWANA YESU ASIFIWE, YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.

Kutokana na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao walitumia mapanga na majambia.

Hata hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi.

Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45), Sadick Yahaya(40), Yasin Rajab(56), Vicent Damon(22), wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika hospital ya wilaya ya Geita.

Hata hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.

Jeshi la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.

Akizungumza kwa njia ya simu na blog hii  mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya kidini.

*TANZANIA YASHINDA TUZO 3 ZA VIVUTIO VYA MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA, NI MLIMA KILIMANJARO, NGORONGORO CRATES NA MBUGA YA SERENGET



 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika picha kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja

Monday, February 11, 2013

mh.lowassa ahudhuria mazishi ya mama yake dr kimei

msiba1 a23b2
Mawaziri wakuu wastaafu Mh Edward Lowassa na Mh Fredrick Sumaye wakijumuka na viongozi wengine katika msiba wa mama yake mkurugenzi mtendaji mkuu wa crdb, dr kimei mwishoni mwa wiki huko Komakundi Marangu Mkoani Kilimanjaro.
msiba2 b42ff
Mh Lowassa akitia saini kitabu cha maomolezi ya kifo cha bibi Eliangichopasia, ambaye ni mama yake mkurugenzi mtendaji wa crdb dr kimei.bibi huyo alifariki wakiwa na umri wa miaka 97

NIGERIA WATWAA RASMI UBINGWA WA AFCON 2013 WAICHAPA BURKINA FASO 1-0

MICHUANO ya 29 ya Kombe la Mataifa Afrika, imemalizika jana usiku kwa timu ya Nigeria kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burkina Faso, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Soccer City.

Sunday, February 10, 2013

HAWA JAMAA BWANA WANATUFANYA WANANCHI MAZUZU KWELI CHEKI WALIVYOMARAFIKI

Spika wa Bunge laTanzania, Anne Makinda akisakata muziki wa dansi na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, mwishoni mwa wiki

RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI DODOMA JIONI HII KUANZA VIKAO VYA CCM J3

 Rais Jakaya Kikwete, akivishwa Skafu na vijana wa Chipukizi CCM, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma leo jioni kwa ajili ya kujiandaa na vikao vua CCM, vinavyotarajia kuanza jumatatu ya wiki ijayo mjini humo.
 Rais Kikwete, akifurahia kwa kupiga makofi wakati vijana wa Chipukizi wakimlaki kwa nyimbo za vijana, uwanjani hapo.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati wa mapokezi ya rais jioni ya leo. Picha na IKULU

Saturday, February 9, 2013

dkt.shein akutana na ujumbe wa kituo cha biashara

IMG_8984
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe
kutoka  Kituo cha Biashara  Duniani (ITC),Jacky Charbonneau,akiongoza
ujumbe wa watu wanne waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya
mazungumzo jana.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

MH MBATIA AFANYA BONGE LA INTERVIEW LEO NA IMPACT FM RADIO 94.4 DODOMA

mh mbatia akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa radio impact ya dodoma leo mara baada ya kufanyanao interview katika taswira yetu

Friday, February 8, 2013

dkt.bilal aendelea na ziara marekani


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza na Seneta, Stive King, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc nchini Marekani, Feb 6, 2013

BREAKING NEWSSS AUWAWA WAKIGOMBANIA MWANAMKE MTAA WA ITIJI NONDE MBEYA

MWILI WA MAREHEMU DANIEL MWASALEMBA 30 UKIWA UMELALA KWENYE MAJANI BAADA YA KUTOLEWA NDANI MAREHEMU AMECHOMWA VISU KISA NI UGOMVI WA KUGOMBANIA MWANAMKE AITWAE ELIZABETH MICHAEL
ANAYEDHANIWA KUSABABISHA KIFO  CHA DANIEL  AMEJULIKANA KWA JINA MOJA TU PETER YEYE NI MWENYEJI WA SUMBAWANGA NA NA NIMWOSH MAGARI YA KAMPUNI YA MABASI YA SUMRY JIJINI MBEYA AKIWA AMEPATA KIPIGO TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI

MSANII MATUMAINI HOI KWA MARADHI ATUA JIJINI TOKA MSUMBIJI

MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
 
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu

MELI YA MV VICTORIA ILIVYNUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO

Maofisa wa kikosi cha zima moto wakijitahidi kuzima moto uliokuwa tayari umesambaa katika maeneo ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.

Meli ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) leo imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo.

Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kusambaa katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya hiyo yaliyopo katika bandari ya Mwanza na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.

ASKOFU THOMAS LAIZER WA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI AFARIKI

 Habari zilizoufikia mTANDAO HUU hivi punde kutoka Jijini Arusha zinaTAarifu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Ask Thomas Laizer, PICHANI  amefariki dunia.

Imeelezwa kuwa  Askofu. Laizer amefikwa na umauti alasiri ya jana katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya jijini Arusha.
 Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea  na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Taarifa zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu.
Pinda alikwenda hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa kuzungumza naye.
Awali ilisemekana kuwa Askofu Laizer amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika Selian kutaka kumwona, lakini jana ilidhihirika kuwa, amelazwa hospitalini hapo.
 FK Blog inatoa pole kwa Waumini na washarika wote wa KKKT nchini kote kufuatia msiba huo mzito ulilolikumba Kanisa la Kilutheri hasa wakati huu ambao kuna mgongano kati ya waumini na Viongozi wa Dayosisi ya Kaskazini Kati.

RAIS KIKWETE AZINDUA VITAMBULISHO VYA TAIFA JIJINI DAR

 Rais Jakaya Kikwete akiangalia Kitambulisho chake cha Taifa baada kuzindua wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo  uliofanyika  leo  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia Kitambulisho chake cha Taifa baada kuzindua wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo  uliofanyika  leo  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

Thursday, February 7, 2013

HATUJANYANG'ANYWA LESENI...BADO TUPO HEWANI".




Kampuni ya ndege ya Fast Jet imezikanusha ripoti kuwa imenyang’anywa leseni yake ya biashara katika nchi kadhaa barani Afrika ikiwemo Tanzania.Kupitia website yake kampuni hiyo imeandika:


Tanzia; askofu katoliki msarikie amefariki dunia

bishop 2a45b
Askofu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Moshi Mhashamu Amedeus Msarikie Amefariki Dunia.

kipanya leo

STARS ILIVYOIADHIBU CAMEROON YA ET'OO 1-0 JANA

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta (kulia) akimtoka beki wa timu ya taifa ya Cameroon kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika jana kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Mbwana Samatta, katika dakika ya 89.
Samatta akiitesa ngome ya Cameroon.
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Erasto Nyoni (kushoto) akiambaa na mpira mbele ya beki wa Cameroon.
Krosi ...........