Saturday, January 5, 2013

MKE WA MAKAMU WA RAIS, MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAMU WA SHULE YA SEKONDARI TAMBAZA

 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi na kujikuwa wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua wafanyalo, badala yake amewambo kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Latifah Nuhu, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Mwinga Gwao, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

KWA HERI SAJUKI

*RAIS KIKWETE AWAONGOZA WANANCHI KUSHIRIKI MAZISHI YA SAJUKI DAR




Rais Jakaya Kikwete, akiwa makaburini Kisutu leo, wakati akishiriki mazishi ya aliyekuwa msanii wa filam, nchini, Sajuki aliyezikwa leo jijini Dar es Salaam.


Tafakuri makini kabla ya mazishi ya Sajuki leo Januari 4, 2013.
Steve Nyerere mwenye kanzu mbele, Tino (nyuma ya Steve) na waombolezaji wengine wakitafakari kabla mwili kufikishwa kwenye makaburi ya Kisutu na kuzikwa jijini Dar es Salaam leo Januari 4, 2013.


Kwaheri jembe letu Sajuki... msanii Ray akitafakari kabla ya kuzikwa kwa Sajuki leo Januari 4, 2013.
Tangulia mwana... sote tuko nyuma yako Sajuki! Jotti akitafakari kabla ya mazishi ya Sajuki leo Januari 4, 2013.

Single Mtambalike 'Richie' (kushoto) naye aliibuka 'kisheikh' kumsindikiza Sajuki leo Januari 4, 2013.  
Chuzi naye alikuwepo na mtoko wake wa Kisheikh.

Kwaheri mwanangu Sajuki... msanii nyota wa filamu, Mzee Chillo naye alikuwapo kumzika Sajuki leo Januari 4, 2013.

Hivi ni kweli umeondoka Sajuki? Siamini!
Mtangazaji Benny Kinyaiya hakubaki nyuma kumsindikiza Sajuki leo Januari 4, 2013.
Msanii Jimmy Mponda a.k.a Jimmy Master alikuwa akimuaga Sajuki kwa staili yake. 
Mhe. Zitto Kabwe (wa pili kushoto) akitafakari jambo na wasanii na waombolezaji wengine katika makaburi ya Kisutu kabla ya kuzikwa kwa Sajuki leo Januari 4, 2013.
Kwaheri kijana wangu....! Msanii nyota wa filamu, Mzee Magali (kulia) akionekana mwenye majonzi tele kabla ya kuzikwa kwa mwenzao Sajuki leo Januari 4, 2013.  
Said Fella (kushoto) na Chege pia walikuwapon
Ni huzuni kubwa kwa kifo cha mpendwa wetu Sajuki... Mungu amlaze pema! Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi Azzan.
Hapa kabla ya kuwasili kwa mwili kwenye makaburi ya Kisutu leo Januari 4, 2013.







Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi tele wa serikali na vyama vya siasa waliojitokeza katika mazishi ya msanii nyota wa filamu nchini, Juma Kilowoko 'Sajuki' aliyefariki juzi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi wengine wa kisiasa walioungana na wasanii na Watanzania wengine kibao katika kumsindikiza Sajuki kwenye nyumba yake ya milele leo baada ya swala ya Ijumaa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mhe. Zitto Kabwe na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi Azzan.
Wasanii wa filamu, muziki na watangazaji wa redio na luninga waliokuwapo ni pamoja na Mzee Magali, Ray, Mzee Chillo, Jotti, Richie, Cheni, Mpoki, Mac Reggan, Chegge, Ben Kinyaiya, Dulla wa East Africa Radio, Said Fella na wengine kibaaaaaaaao....!
Shughuli zote za msiba wa Sajuki zilifanyika nyumbani kwake Tabata Bima kabla baadaye jeneza lake kupelekwa katika makaburi ya Kisutu na kuzikwa mara tu baada ya swala ya Ijumaa.
Marehemu ameacha mke ambaye ni msanii wa filamu pia aitwaye Wastara na mtoto mmoja.
Innalillahi Wa Innaillaihhi Rajjiuuun...(Sisi ni wa Mwenyezimungu, kwake yeye tutarejea na atatupa jaza yake)... Aaaamin!!

Wednesday, January 2, 2013

KWA HERI SAJUKI


Wednesday, January 2, 2013

*WAZIRI FENELLA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA SAJUKI, SHUGHULI ZA MSIBA ZINAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA BIMA


Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Msanii Sajuki, wakiwa katika maombolezo ya msiba wa kipenzi chao, nyumbani kwa marehemu Tabata Bima, Dar es Salaam, leo.

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangaraamewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo  katika tasnia ya filamu hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt. Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja  na Revenge  ya Kampuni ya RJ .
Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers  kwa kushirikiana na Shija  Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk 
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na  furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli  huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.
Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen
********************************
MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI YA HABARI YA MSIBA WA SAJUKI,TABATA.
 Dada wa marehemu Sajuki akilia kwa uchungu.
Bibi wa marehemu Sajuki akiwasili msibani leo.
 
Pichani juu ni baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki', Tabata- Bima jijini Dar es Salaam. 
Sajuki amefariki dunia leo alfajiri akiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili ambapo alikuwa akitibiwa

Tuesday, January 1, 2013

HAPPY NEW YEAR 2013



MAKE THE HISTORY

 HONGEREN WOTE MLIOFIKA MWAKA HUU
HUYU JAMAA ANAJUA MAANA YA HAYA MANENO JAMANI HEBU NISAIDIENI

WAZEE WA KAKOLA-KAHAMA HAPA NI KAZI TUUU

 MZEE WA KAZI DAUDI AKIWA KATIKA TAFAKARI ZITO
SAFARI INAENDELEA HAPA

WAKAZI WA MGODI WA KAKOLA WILAYANI KAHAMA WASHEREHEKEA MWAKA MPYA NA WINDHOEK LAGER

 VIJANA WA MGODINI WAKIUPOKEA MWAKA MPYA NA WINDHOEK BEER
 RAHA ZINAENDELEA KAMA KAWAIDA

 BAADA YA KUFURAHI NA WINDHOEK ANACHEK CAMERA YETU
MZIGO NI TAMU UMETEMBEA VIBAYA CHEK CHUPA VYUPA HIZO WINDHOEK TAMU BWANA