Chama cha mawakili nchini Kenya LSK kimemkosoa rais Uhuru Kenyatta wa
Kenya dhidi ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi
wa kubatilisha uchaguzi wake.
Rais Kenyatta alitoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wafuasi wake katika soko la Burma mjini Nairobi siku ya Ijumaa muda mfupi baada ya mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufutilia mbali uchaguzi wake.
Amesema kuwa rais Kenyatta anapaswa kulinda haki ya majaji na idara yote ya mahakama.
Bwana Okero amesema kuwa ijapokuwa rais huyo ana haki ya kutoa maoni yake anafaa kutoa maoni yanayostahiki.
''Haki yake inafaa kuheshimu, kukubali na kulinda haki za jaji mkuu na kila jaji wa mahakama ya juu chini ya kifungu cha sheria cha 28''.
''Matamshi hayo yanakiuka na yanashutumiwa na chama cha mawakili Kenya LSK'', aliongezea.
Kiongozi huyo wa LSK amesema kuwa mahakama hiyo ilifanya wajibu wake na kuwaonya viongozi wengine dhidi ya kuwatishia majaji.
Mahakama ya juu inayoongozwa na jaji Maraga ilifutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kutokana na dosari iliotekelezwa na tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC
No comments:
Post a Comment