Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai,
amesema ana uwezo wa kumzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe
kuzungumza mpaka mwisho wabunge, kwani hawezi kupambana naye.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe
hawezi na hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha
na aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi
kufanana naye na kila mtu ana muda wake, kama ambavyo Spika wa bunge
aliyepita mama Anna Makinda alivyokuwa na muda wake kuliongoza bunge
hhilo
“Hawa ni watu nawaheshimu sana na wamenilea sana na ni sehemu
nilipofika hapa leo. Utanilinganishaje mimi na milima mikubwa kama
Kilimanjaro? Hata siku moja sikio haliwezi kuzidi sikio,” amesema.
Amesema katika Bunge la 9 Zitto aliwahi kupeleka hoja ya Mgodi wa
Buzwagi ambayo ilikataliwa na Bunge lakini ikazuka hoja ya kimaadili
ambapo alihukumiwa hapo hapo.
“Alihukumiwa hapo hapo akapigwa miezi mitatu. Mnatakaniende mkuku
mkuku kama lile la Bunge la tisa nifanane na mzee Sitta? Hilo pia
naliweza kwa nini mnaalika matatizo nashangaa unapambana na Spika,”
amesema.
“Ninauwezo wa kupiga marufuku kuzungumza hadi miaka yote mitano iishe
hauna pa kwenda, hakuna cha swali, nyongeza wala kuzungumza utanifanya
nini?Amemtaka kupambana na mtu mwingine lakini sio yeye.”Kwa haya ya
Spika sina sababunayo lakini ya kulidharau Bungehayo sitaweza
kuyavumilia nitalinda mihimili huu kwa nguvu zangu zote,” amesema.
Amesema hawawezi kuacha wabunge kulidhalilisha Bunge na kuhoji kwamba
watachukuliaje Watanzania wengine watakapolidhalilisha Bunge.Amesema
hilo kosa la pili kwa Zitto na kuagiza liende katika kamati ya maadili.
“Tutaenda sambamba mguu kwa mguu hadi kieleweke,” amesema juzi Spika
Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili kutoa
maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe
kumjibu kuwa mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge
No comments:
Post a Comment