Tuesday, November 28, 2017

MEYA IRINGA NA MAKADA WATANO CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe mwenye koti la suti akitolewa mahabusu kwenda mahakamani kusikiliza kesi ilitolewa ikimkabili ya kutishia kuua kwa bastola 
Meya kushoto akiwa chini ya ulinzi
MSTAHIKI meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe (chadema) amepandishwa mahakamani kwa kosa la kutishia kumuua katibu wa UV CCM wilaya ya Iringa mjini Alphonce Myinga wakati wa zoezi la uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kitwiru.

Meya Kimbe alifikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Iringa John Mpitanjia leo majira ya saa 3 asubuhi na kusomewa shitaka hilo la jinai kesi namba 189 /2017.

Akisoma shitaka hilo wakili wa jamhuri Allysniki Mwinyiheni alisema kuwa Kimbe alitenda kosa hilo Novemba 26 mwaka huu katika eneo la Kitwiru mjini Iringa kwa kumtishia kumuua kwa bastola Myinga .

Hata hivyo Kimbe alikana kosa hilo na kesi hiyo kuja tena mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa Desemba 12 mwaka huu na meya huyo yuko nje kwa dhamana baada ya mahakama kukubali kumpa dhamana .

Wakati huo huo makada watano wa Chadema jana walifikishwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Richard Kachele kwa makosa matatu likiwemo la unyang’anyi .

Wakili wa jamhuri alisema mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao Martha Robarth , Leonard Kulujila, Christopher Gerlad,Samweli Nyanda na Asau Bwile kwa pamoja wanashitakiwa kwa makosa matatu ambayo ni kujeruhi, Unyang’anyi wa kutumia nguvu na utekaji .

Kuwa tukio hilo walilifanya Novemba 19 mwaka huu eneo la Kitwiru kwa kumteka Dikri Frank kada pamoja na kumteka walimpokonya simu yake ya mkononi yenye thamani ya shilingi 100,000 pamoja na kadi ya CCM moja.

Washitakiwa hao ambao wanatetewa na wakili CHarzy Luoga walikana kosa hilo na kunyimwa dhamana kutokana na kosa la unyang’anyi katika kesi hiyo namba 190/2017 kutokuwa na dhamana .

Wakili wa washitakiwa hao aliiomba mahakama kuagiza wapelelezaji wa kesi hiyo kufanya haraka kwani wateja wake wana maumivu na mmoja hawezi hata kusimama baada ya kuumizwa na polisi wakati walipokamatwa .

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 12 mwaka huu itakapofikishwa tena kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote walirudishwa mahabusu

Thursday, September 14, 2017

VITA YA SPIKA JOB NDUGAI NA MH ZITO KABWE SASA YAFIKIA HAPA.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, amesema ana uwezo wa kumzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuzungumza mpaka mwisho wabunge, kwani hawezi kupambana naye.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi kufanana naye na kila mtu ana muda wake, kama ambavyo Spika wa bunge aliyepita mama Anna Makinda alivyokuwa na muda wake kuliongoza bunge hhilo
“Hawa ni watu nawaheshimu sana na wamenilea sana na ni sehemu nilipofika hapa leo. Utanilinganishaje mimi na milima mikubwa kama Kilimanjaro? Hata siku moja sikio haliwezi kuzidi sikio,” amesema.
Amesema katika Bunge la 9 Zitto aliwahi kupeleka hoja ya Mgodi wa Buzwagi ambayo ilikataliwa na Bunge lakini ikazuka hoja ya kimaadili ambapo alihukumiwa hapo hapo.
“Alihukumiwa hapo hapo akapigwa miezi mitatu. Mnatakaniende mkuku mkuku kama lile la Bunge la tisa nifanane na mzee Sitta? Hilo pia naliweza kwa nini mnaalika matatizo nashangaa unapambana na Spika,” amesema.
“Ninauwezo wa kupiga marufuku kuzungumza hadi miaka yote mitano iishe hauna pa kwenda, hakuna cha swali, nyongeza wala kuzungumza utanifanya nini?Amemtaka kupambana na mtu mwingine lakini sio yeye.”Kwa haya ya Spika sina sababunayo lakini ya kulidharau Bungehayo sitaweza kuyavumilia nitalinda mihimili huu kwa nguvu zangu zote,” amesema.
Amesema hawawezi kuacha wabunge kulidhalilisha Bunge na kuhoji kwamba watachukuliaje Watanzania wengine watakapolidhalilisha Bunge.Amesema hilo kosa la pili kwa Zitto na kuagiza liende katika kamati ya maadili.
“Tutaenda sambamba mguu kwa mguu hadi kieleweke,” amesema juzi Spika Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili kutoa maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe kumjibu kuwa mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge

YUSUPHU MANJI SASA RASMI YUKO HURU.


Image result for manji yusuf mahakamani
KISUTU: Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yake.
Manji na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali.
Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

Tuesday, September 12, 2017

RAIS DKT MAGUFULI AMJULIA HALI MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA ALIYEJERUHIWA KWA RISASI.


LU (2)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto Nathan Martin  wakati akitoka kumjulia hali Meja jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

LU (4)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo baada ya kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na mguuni wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
LU (5)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu  Aloys Konolipa wa Shule ya Msingi Kidugalo wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani alipopita kuwapa pole wagonjwa wengine baada ya kumjulia hali Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni.
LU (7)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba akielezea alivyoshambuliwa kwa  risasi mkononi, tumboni na mguuni  wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam
LU11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe,  Brigedia Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba na wauguzi wakiomba dua wakiongozwa na Mama Margareth Vicent Mritaba katika  hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa Meja Jenerali Mritaba akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
LU12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe wakiangalia majeraha aliyopata Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS AZINDUA PROGRAMU YA MABORESHO YA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA.

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango wakati akiwasili kwenye uzinduzi wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 – 2021/22 katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

POLISI WAKANUSHA KUMPELEKA KACHERO KUMFUATA LISSU NAIROBI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA
 
Anuani ya
Simu “MKUUPOLISI”
Ofisi ya
Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022)
2110734
Makao Makuu
ya Polisi,
Fax Na.
(022) 21355
S.L.P. 9141,

DAR
ES SALAAM.



12/09/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za karibuni kumejitokeza vitendo vya baadhi ya watu kutumia majina ama
picha za watu na kuwahusisha na matukio ya kihalifu au matukio yanayohusiana na
uhalifu kwa lengo la kujipatia umaarufu, kuwachafua watu hao au kuwakosanisha
na jamii inayowazunguka.


Mnamo tarehe 11.09.2017 kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa picha ya askari wa
Jeshi la Polisi akihusishwa na muendelezo wa tukio la kujeruhiwa kwa risasi kwa
Mhe. Tundu Lissu (MB) ambapo taarifa hiyo ilimtambulisha askari huyo kuwa ni
kachero wa Kitengo cha Interpol na kwamba yupo jijini Nairobi nchini Kenya
akifuatilia taarifa za Mhe. Lissu.
Jeshi
la Polisi linapenda kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na ni za uongo
zenye lengo la kumchafua askari huyo na Jeshi la Polisi kwa ujumla. Askari huyo
hayupo Nairobi kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika ilipigwa hapa nchini
tarehe 07.01.2017 kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake.
Kuhusiana
na safari ya Nairobi, askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa kozi ya kimafunzo
kuanzia tarehe 04.09.2017 na kurejea tarehe 08.09.2017, huku Mhe. Lissu
akipatwa na mkasa wa kujeruhiwa kwa risasi Tarehe 07.09.2017 na kusafirishwa
kwenda Nairobi usiku wa kuamkia tarehe 08.09.2017.
Jeshi
la Polisi linakemea vikali kitendo hiki chenye lengo la kumharibia maisha yake
askari wetu, na linawataka wale wote waliohusika kusambaza au kutajwa katika
taarifa hizo kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa
ajili ya mahojiano. Vilevile tunatoa onyo kwa wote wanaofikiri kuwa wanaweza
kukaa na kupika habari ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua
upande wa serikali.
Suala
hili la Mhe. Lissu lipo chini ya uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na
tukio hili na hatimaye kuwafikisha mahakamani. Ni vema wananchi na wanasiasa
wakaliacha Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake bila kuliingilia ili kuweza
kupata ukweli wa jambo hili.
Jamii
itambue kuwa Jeshi la Polisi linafanyakazi kwa mujibu wa Sheria, kanuni na
taratibu za Nchi na kamwe halifanyi kazi kwa kuvizia. Endapo mtu yeyote
anahitaji taarifa, tunayo mifumo yetu rasmi inayotuwezesha kupata taarifa
tuzitakazo kupitia uhusiano tulionao ndani na nje ya nchi.
Jeshi
la Polisi kupitia Kitengo cha upelelezi wa makosi ya mitandao (Cyber Crime
Investigation Unit) linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na
kusambaa kwa taarifa hizi za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Jeshi
la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na
badala yake mitandao hii itumike kwa ajili ya kuelimisha na kuihabarisha jamii
juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
 
 
 
 
 
Imetolewa na:
Barnabas David
Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
                                                                   Makao Makuu ya
                                                                       Polisi

Thursday, September 7, 2017

RAIS WA TLS NA MWANASHERIA WA CHADEMA( MB) TUNDU LISU ASHAMBULIWA KWA RISASI NA WATU WASIO JULIKANA.

TAARIFA zilizotufikia ni kwamba Rais wa chama cha mawakili Tanganyika (TLS) Tundu Lisu amepigwa risasi tano na watu wasiojulikana na amekimbizwa hospitali

Tukio hilo limetokea mjini Dodoma mchana wa leo nyumbani kwake Area D akiwa ktk gari yake akijiandaa kwenda Bungen

WAZIRI WA TAMISEMI MH SIMBACHAWENE AJIUZULU UWAZIRI .


Image result for sIMBACHAWENETaarifa  zilizoufikia mtandao  huu  wa matukiodaima  hivi  punde  zinaeleza  kuwa  waziri  wa Tamiseni George  Simbachawene  amejiuzulu  nafasi yake  baada ya  rais  Dkt  John Magufuli  kutaka wajiondoe katika nafasi zao  kufuatia  kutajwa  kwenye ripoti ya madini  na kamati iliyoundwa  kuchunguza suala  hilo.

Waziri  huyo  amedaiwa  kuachia  nafasi yake  leo huku  mawaziri  wengine wapo  mbioni kuachia nafasi  zao  au  kusubiri  kutumbuliwa

Sunday, September 3, 2017

MAWAKILI KENYA WAMCHIMBIA MKWARA RAIS KENYATA.

Rais wa LSK Isaac Okero                  Rais wa LSK Isaac Okero                


Chama cha mawakili nchini Kenya LSK kimemkosoa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya dhidi ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake.
Rais wa LSK Isaac Okero katika taarifa siku ya Jumamosi alimkosoa rais Kenyatta kwa kumtaja jaji mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa ''wakora''.
Rais Kenyatta alitoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wafuasi wake katika soko la Burma mjini Nairobi siku ya Ijumaa muda mfupi baada ya mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufutilia mbali uchaguzi wake.

Bwana Okero alisema: Matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais Uhuru Kenyatta achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya.
Amesema kuwa rais Kenyatta anapaswa kulinda haki ya majaji na idara yote ya mahakama.
Bwana Okero amesema kuwa ijapokuwa rais huyo ana haki ya kutoa maoni yake anafaa kutoa maoni yanayostahiki.

''Haki yake inafaa kuheshimu, kukubali na kulinda haki za jaji mkuu na kila jaji wa mahakama ya juu chini ya kifungu cha sheria cha 28''.

''Matamshi hayo yanakiuka na yanashutumiwa na chama cha mawakili Kenya LSK'', aliongezea.
Kiongozi huyo wa LSK amesema kuwa mahakama hiyo ilifanya wajibu wake na kuwaonya viongozi wengine dhidi ya kuwatishia majaji.
Mahakama ya juu inayoongozwa na jaji Maraga ilifutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kutokana na dosari iliotekelezwa na tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC

Wednesday, July 26, 2017

MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SCAUT MJINI DODOMA NA KUWAVISHA NISHANI VIONGOZI WASTAAFU

 Mama FATMA KARUME akivishwa nishani ya heshima kwa niaba ya hayati ABEID  AMAN KARUBE.
 Rais mstaafu wa tanzania wa awamu ya nne MH JAKAYA KIKWETE akivishwa nishani ya heshima na makamu wa rais MH SAMIA SULUHU.
 Rais mstaafu wa zanzibar akivishwa nishani.
 Rais mstaaf wa awamu ya pili MH ALLY HASSAN MWINYI akivishwa nishani ya heshima na makamu wa rais MH SAMIA SULUHU.
 Makamu wa rais MH SAMIA SULUHU akimvisha nishani ya heshima waziri mkuu staafu MH SALIMU AHMED SALIMU katika maadhimisho ya miaka 100 ya SCAUT TANZANIA.
Makamu wa rais mh SAMIA SULUHU HASAN akiongea katika maadhimisho ya miaka 100 ya SCAUT mjini dodoma.

WALIOFUKUZWA UANACHAMA NA CUF WAPOTEZA NA UBUNGE WAO.



Thursday, July 20, 2017

RAIS WA BURUNDI MH:PIERRE NKURUNZINZA AFANYA ZIARA YA SIKU MOJA TANZANIA.

Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwapungia wananchi alipowasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwa wamesimama wakipokea salamu za heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama.
Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akikagua graride la lililoandaliwa na jeshi la ulinzi la Tanzania JWTZ katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Kumpokea katika Uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye uwanja wa Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta Jambo na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza Mara baada ya kumpokea katika Mji wa Ngara kwenye uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza kwa maongezi mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo maalum ya kiserikali na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza na ujumbe wake Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza pamoja na mama Janeth Magufuli katika Maongezi.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchimwa mji wa ngara wakati wakiwasili katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Umati wa ananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kusikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa posta mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza katika uwanja wa Lemela Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017 baada ya kumaliza ziara yake Rasmi ya kiserikali Nchini. PICHA NA IKULU.