Maelezo yaliyoandikishwa na Aika polisi yalidai kwamba Lady Hanifa alifika kwenye baa hiyo ambayo ndani yake anamiliki jiko la chakula na kuelezwa kwamba, siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na deni na alipofika tu, Aika alimkumbushia ndipo balaa lilipoanza.
Ilisemekana kwamba Aika alimfuata na kumwambia kuwa jana yake alikuwa akidaiwa bia moja tu ya baridi aliyokuwa amekopa, kitendo kilichompandisha hasira na kuona kama amefedheheshwa kudaiwa mbele za watu.
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth.
Iliendelea kudaiwa kwamba katika
purukushani hizo, Aneth aliyekuwa ameshika kisu alimchoma nacho Aika
tumboni, kichwani, mikononi huku Lady Hanifa akimuunguza shingoni kwa
kutumia upawa wa chipsi uliokuwa na mafuta ya moto kisha wakakimbia.
Habari zilieleza kwamba baada ya hapo Hanifa na Aneth walikimbilia
Kituo cha Wazo Hill kutoa taarifa lakini muda mfupi wasamaria wema
walifika katika kituo hicho wakiwa na Aika aliyekuwa ametapakaa damu
mwili mzima.Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
No comments:
Post a Comment