Msemaji wa Rais alikana kuwa gari hilo lilikuwa limeibwa
Maafisa
wakuu kutoka shirika la polisi wa kimataifa, Interpol amethibitisha kuwa
gari la ulinzi wa rais Uhuru Kenyatta lililoibwa mjini Nairobi wiki
jana limepatikana nchini Uganda.
Kwa sasa gari hilo limepelekwa mjini Kampala.
Gari hilo aina ya BMW liliibwa siku ya Jumatano usiku mjini Nairobi. Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na wizi huo.
Mkurugenzi wa polisi wa kimataifa Interpol nchini Uganda Assab Kasingye aliambia BBC kuwa gari hilo litarudishwa Nairobi.
Gari hilo liliibwa na watu waliokuwa wamejihami Jumatano wiki jana.
Hata
hivyo msemaji wa serikali Manoah Esipisu alikanusha habari hizo akisema
kuwa gari lililoibwa halikuwa na ulinzi wa Rais Kenyatta bali lilikuwa
gari kuu kuu la polisi.
Lakini
lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi aliyeripoti kuwa gari hilo ni
mmoja ya magari ya ulinzi wa Rais.Afisa huyo wa polisi pia alisemekana
kuwa mmoja wa maafisa wa polisi wa ulinzi wa Rais.
Tukio la
wizi wa gari hilo, lilisababisha taharuki miongoni mwa maafisa wa ulinzi
kwa sababu magari ya ulinzi wa Rais yenyewe yanapaswa kuwa na ulinzi
mkali.
Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa visa vitatu vya wizi wa magari huripotiwa mjini Nairobi kila siku.
Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi vya wizi wa magari ambapo mtu yeyote anaweza kuathirika.
No comments:
Post a Comment