Monday, July 29, 2013

MABANGO YA TIGO NA VODA DODOMA KUSHUSHWA CHINI NA HALMASHAURI YA DODOMA.


MADIWANI wa halimashauri ya manispaa ya Dodoma wamemtaka muwekezaji
anayeshughurikia mabango ya matangazo yote ya kampuni za simu
yanayowekwa kwenye taa  za barabarani ayashusha ndani ya siku saba.

Madiwani hao walifikia makubaliano ya kuchukua hatua hiyo ya kumuondoa
mwewekezaji huyo kwenye Baraza  la kawaida la madiwani lililokutana
ili kujadili kwa kina maswala mbalimbali ambayo yamekuwa yamekuwa
kikwazo katika mapato halimashauri yao.




Madiwani wa Halimashauri ya manispaa ya Dodoma wakiwa katika ukumbi wao wa mikutano wakifuatilia hoja mbalimbali kwa umakini wakati walipokuwa kwenye mkutano wao wa kawaida juzi ambapo waliazimia kuyashusha mabango yote ya Voda, Tigo na Artel kwenye taa za barabarani.



Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini DKT David Malole akifafanua jambo alipokuwa akiongea na madiwani kwaenye mkutano wao wa kawaida.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma akizungumza jambo na madiwani waliokuwa kwenye Baraza maarum kujadili hoja maarum na kuzipatia majibu.


wataalamu wa fani mbalimbali wa manispaa hiyo wakifuatilia agizo la madiwani kwa makini sana

Thursday, July 25, 2013

MTOTO Magge Fred 8 amejeruhiwa kichwani na kung'atwa kwa meno Mgongoni na mabegani na Mama yake mzazi kwa sababu aliiba fedha na kununulia Chips bila ruhusa.


Terethia Fidelis aliyebeba mtoto mgongoni akisindikizwa na umati wa watu toka ofisi ya mkuu wa mtaa alipokuwa akihijiwa kuhusu tuhuma yake ya kumpiga, kumpasua kichwani na kumng'ata na meno mgongoni mtoto wake Magge Fred 8.


Mtuhumiwa Theresia Fidelis akipanda Kwenye gali la polisi baada ya kutuhumiwa kumpiga, kumpasua kichwa na kung'ata kwa meno Mtoto wa Magge Fred 8 mwanafunzi wa Darasa la pili Mnadani Dodoma.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume kata ya mnadani manispaa ya Dodoma  Matwiga Kyata akionyesha moja ya majeraha ya kichwani na Mgongoni, aliyojeruhiwa mtoto MaggE Fred 8, kipogo hicho kinadaiwa kufanywa na mama yake mzazi.
                         [PICHA NA JOHN BANDA]

Tuesday, July 23, 2013

AGNESS MASOGANGE KUPANDISHWA TENA KIZIMBANI AUGOST 13,2013.

Msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya teyari walishapanda kizimbani, na kesi yao inatarajiwa tena kusomwa 13 Agoust mwaka huu nchini humo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili teyari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.

Alisema kuwa kutokana na ushahidi bado haujakamilika wadada hao wanatarajia kupanda kizimbani tena tarehe 13 mwezi Agoust mwaka huu.

Kamanda Nzowa aliweka wazi kuwa nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo hilo, hivyo anaamini kuwa kila jambo litaenda sawa.

"Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi" alisema Nzowa.

Wadada hao ambao walikamatwa nchini Afrika kusini wakitokea Tanzania wakiwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya ambazo zilifahamika kuwa ni  Chemical bashirifu, ambazo hazina matumizi nchini.

Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo wakiwa shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8 wakitokea Tanzania