Thursday, July 10, 2014

MWANAMKE AGONGWA NA KUFA PAPO HAPO KARIBU NA UKUMBI WA BUNGE MJINI DODOMA

Watu wakiuangalia mwili wa mtu ambaye hakufahamika jina jina lake baada kugongwa na gari lisilofahamika na kufa papo hapo, katika eneo la bohari ya mkoa kati ya bunge na kituo cha mabasi yaendayo mikoani,barabara ya morogolo Dodoma
polisi wa usalama barabarani wakisaidiana na wananchi kuupakia mwili wa mtu aliyekutwa amegogwa na kufa papo hapo na gari ambalohalikujulikana baada ya kukimbia katika barabara ya morogolo Dodomakaribu na jengo la bunge la Tanzania.

PICHA NA JOHN BANDA

Wednesday, July 9, 2014

MASHABIKI WA BRAZIL WAPELEKA HASIRA ZAO KWA KUCHOMA MOTO MABASI BAADA YA KUPIGWA 7-1





Basi lililochomwa na mashabiki wa Brazil waliokuwa na hasira likiteketea kwa moto.

Vikosi vya zimamoto vikijaribu kuzuia moto huo.

Taswira baada ya basi hilo kuteketea kwa moto.

Polisi wakimdhibiti shabiki huko Belo Horizonte baada ya mechi ya nusu fainali.

Mashabiki wa Brazil wakiwa na majonzi baada ya kipigo cha 7-1.
BAADA ya kubugizwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014, mashabiki wa Brazil wameamua kuchoma moto basi.
 
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huko Sao Paulo nchini humo baada ya mechi hiyo iliyopigwa Belo Horizonte.
 
Mashabiki walichukua hatua hiyo kutokana na hasira za timu yao kuondolewa katika michuano hiyo inayofanyika nyumbani kwao

KIBAKA ALA KICHAPO BAADA YA KUSKWAPUA SH MIL 5 KWA MTEJA WA BENKI DAR .



Askari kanzu (kulia), akimpeleka kituo cha Polisi Kati, kijana aliyedhaniwa kumkwapua mtu aliyetoka benki ya NBC katika ya Jiji leo mpita njia fedha zilizotajwa kufikia sh. mil. 5, maeneo ya Mtaa wa Samora, Dar es Salaam akiwa na wenzake ambao walifanikiwa kukimbia na fedha hizo. (PICHA NA KASSIM MBAROUK)

Tuesday, July 8, 2014

WASHUKIWA WAWILI WAKAMATWA KWA KULIPUA BOMU MGAHAWANI ARUSHA .


Watu wawili wamekamatwa na Polisi wakihusishwa na shambulio la bomu lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian cuisine' jijini Arusha. 

Shambulizi hilo liliyokea Jana siku ya jumatatu saa nne usiku.
Watu wasiojulikana walirusha bomu ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja kati yao akiwa na majeraha makubwa.

Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20 wanazuiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.

Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.

Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.

Monday, July 7, 2014

MABOMU YALIPUKA ARUSHA TANZANIA

Photo
Kwa habari tulizozipata leo ni kwamba majira ya saa kumi jioni kumetokea mlipuko wa mabomu katika mitaa ya Ngarenaro nyuma ya soko la Kilombero.
 Chanzo cha mlipuko huo hakijajulikana hadi hivi sasa.
Bomu hilo limesababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo huku majeruhi hadi hivi sasa wako katika hospitali ya Mount Meru

KUNDI LA MRC LASHUTUMIWA KWA MASHAMBULIZI NCHINI KENYA.

Polisi wa kagua mwili wa mtu aliyeuliwa na washambulizi katika kijiji cha Hindi, Lamu Kenya
Polisi nchini Kenya inaeleza kwamba washambuliaji wamewauwa watu 29 huko Lamu na Tana River. Polisi inasema wahusika wa shambulio hilo ni wanachama wa kundi la Mombasa Republic Council-MRC ingawa kundi la wanamgambo wa Al-Shabab kutoka Somalia linadai kuhusika.
Vyombo vya habari vya kenya vinamnukuu naibu inspeka mkuu wa polisi Grace Kaindi akisema jumapili kwamba watuhumiwa wakuu ni wanachama wa MRC na kwamba malengo yao huwenda yakawa ni ya kisiasa, kikabila au suala la mashamba. "Kundi la kiasi cha watu 30 hadi 50 waliwashambulia maafisa wa polisi waliokua katika kituo cha polisi cha Gamba . kulikuwepo na mashambulizi makali. Na kundi moja la washambuliaji walifanikiwa kuingia ndani ya kituo na kuwauwa watu watano waliokua wanashikiliwa huko. Afisa moja wa polisi aliuliwa na wawili kujeruhiwa

Tuesday, July 1, 2014

Tume ya uchaguzi ya Taifa katika maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kula kwa kutumia mfumo wa Teknojia wa BIOMETRIC VOTER REGISTRATION [BVR] kwa waandishi wa habari Dodoma

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliopo mkoa wa Dodoma
wakiwa katika ukumbi wa manispaa kufuatili semina iliyotolewa na Tume
ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu Maboresho ya kudumu ya Daftari la wapiga kura

Jaji Mkuu Mstaafu wa Nzanzibar ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa Uchaguzi  Mhe. Hamid Mohamoud Hamid akifungua Mafunzo
kwa waandishi wa Habari wa mkoa wa Dodoma kuhusu Maboresho ya kudumu
ya Daftari la wapiga kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Kushoto Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Tume hiyo Oigenia Mpanduji,.
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Mhandisi Lusako
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Tume ya uchaguzi ya Taifa
Oigenia Mpanduji akitoa ufafanuzi wa jambo alipokuwa akitoa mada kwa
waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kuhusu, Maandalizi ya Maboresho
ya Daftari la kudumu wapiga kura kwa kutumia Teknolojia ya Biometric
Voter Registration [BVR]  leo.

PICHA NA JOHN BANDA