Tuesday, March 25, 2014

TBS YAWAFUNDA WALEMAVU WASIOSIKIA (VIZIWI) KUTOKA MIKOA YA DODOMA,SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA JUU YA UZALISHAJI WA BIDHAA KWA KUZINGATIA VIWANGO VYA UBORA

Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakiwashangilia kwa lugha ya alama wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (hawapo pichani) wakati wakijitambulisha kwenye semina iliyoandaliwa na TBS kwa ajili ya kuwafunda walemavu hao masuala ya viwango vya ubora  katika shughuli za,uzalishaji  iliyofanyika mapema Leo hii.
Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akiwasisitizia walemavu wasiosikia (viziwi) kuzingatia ubora wa viwango kwenye bidhaa wanazozalisha kwenye sekta ya kilimo, ufugaji nyuki na mifugo na ujasiriamali ili kunufaika na masoko ya kimataifa wakati akifungua semina kwa walemavu hao juu ya masuala ya ubora wa viwango  iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS, semina hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma, wengine pichani ni maafisa kutoka TBS.
Baadhi ya wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji katika sekta za kilimo, ufugaji mifugo na nyuki na ujasiriamali kutoka mikoa ya Dodoma, singida, Tabora na shinyanga wakishangilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na mkuu wa mkoa Dodoma na kutafsiriwa kwa lugha ya alama kwenye semina ya masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS mapema Leo mjini Dodoma.
Picha ya pamoja baina ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema Nchimbi, wataalamu wa masuala ya viwango vya ubora kutoka TBS na walemavu wasiosikia (viziwi) kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na shinyanga muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua semina kwa walemavu hao juu ya  masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS na kufanyika mapema Leo Jumatatu Machi 24, 2014.


No comments:

Post a Comment