Na John Banda,Dodoma.
BAADA ya hivi karibuni Mbuge
wa jimbo la Dodoma mjini Dkt David Malole kutangaza kujitoa kwenye bodi ya CDA,
Nae Mjumbe wa NEC ya chama cha mapinduzi [CCM] Anthony Kanyama agongelea
msumali wa moto
Mnec Huyo aliugongomelea msumari huo wa moto baada ya kuwataka Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuikataa Rasimu ya Muswada wa Sheria ya kutaka Mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA) iendelee kuwepo.
Mnec Huyo aliugongomelea msumari huo wa moto baada ya kuwataka Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuikataa Rasimu ya Muswada wa Sheria ya kutaka Mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA) iendelee kuwepo.
Agizo hilo alilitoa
kwenye Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM alipokuwa
akizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Mji Mwema Kata ya Chang’ombe Manispaa
ya Dodoma .
Kanyama aliwataka kupinga
suala hilo na kudai kuwa Mamlaka hiyo tayari imeshaandaa rasimu ya
Muswada wa Sheria yenye mapendekezo yake ya kutaka kuendelea na wanataka
kupeleka Bungeni ili uweze kusomwa licha ya wabunge na madiwani ambao
ndio walengwa kutoshirikishwa.
Alisema pamoja na wabunge na
madiwani kuwa ndio wahusika wakuu, cha kushangaza hawakushirikishwa na badala
yake walishirikishwa wadau wengine wasiojua kero ambao sio wakazi wa Manispaa .
“ CDA ilianzishwa Mwaka 1973
kwa kupigiwa kura na Mikoa yote ya nchi nzima ambapo Mikoa 18 iliunga
mkono na Mikoa mitatu ilipinga lakini Wananchi hawakushirikishwa, cha
kushangaza Mamlaka hii imekuwa ikijifanyia mambo kiholeala tena kwa
uzembe,”Alisema Kanyama.
Mjumbe huyo wa NEC alisema
kuwa kufuatia kuwepo kwa suala hilo,tayari Baraza la Madiwani kwa kushirikiana
na Wabunge wa Manispaa hiyo imeandaa hoja 78 kwa ajili ya kuwapelekea Mamlaka
CDA .
Ili iweze kuwajibu na endapo Mamlaka hiyo itawapa majibu ambayo hayaridhishi watalazimika kwenda kwa Rais ambaye ndio mwamuzi wa mwisho juu ya Ardhi.
Ili iweze kuwajibu na endapo Mamlaka hiyo itawapa majibu ambayo hayaridhishi watalazimika kwenda kwa Rais ambaye ndio mwamuzi wa mwisho juu ya Ardhi.
Kanyama ambaye pia ni
Mwanasheria wa CCM, alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha Mamlaka hiyo
kuwafanya wakazi wa Manispaa ya Dodoma kama kaburi kutokana na unyanyasaji wa
kuwabomolea Nyumba zao ikiwemo kuwanyang’anya maeneo yao huku ikiwapunja fidia.
Awali Wakazi wa
Kitongoji cha Mji Mwema kupitia Katibu kata wa CCM Chang'ombe Suleiman Mringo
wakitioa malalamiko yao mbele ya Mjumbe huyo wa NEC,walisema Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA),imekuwa ikiwafanya waishi kama Wanyama wa
porini kutokana na kuhofia kubomolewa Nyumba zao kwa madai ya kuambiwa
kuwa ni wavamizi.
“Hivi sasa tunaishi kama
digidigi wakati maeneo yetu haya tayari tuna Miundombinu mbalimbali
ikiwemo Shule ya Msingi na Sekondari na watoto wetu wanasoma je hii
ni haki? tutaenda wapi ,kwa maana hiyo tunaiomba Serikali itusaidie tuweze kupimiwa
maeneo yetu,” Walisema.
Mjumbe wa NEC ya CCM Taifa
Anthony Kanyama anayecheka katikati akiwa na vingozi wa chama hicho wa kata ya
Chang'ombe walipokuwa kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya CCM.
Akinamama wakazi wa kitongoji cha Mji mwema
manispaa ya Dodoma wakiselebuka wakati walipokuwa wakumsindikia Diwani wao Bakari
Fundikila aliyekuwa akijiandaa kuwasilisha ujumbe kwa mgeni rasimi.
No comments:
Post a Comment