Mmoja wa viongozi wa
waendesha Bodaboda wanao toa huduma ya usafiri
ndani na n je ya chuo hicho akiwagawia funguo za pikipiki zao baada
ya jana kutotoa huduma hiyo kwa zaidi ya saa 7 wakijadili nini cha
kufanya baada ya kutakiwa kutopakilia abiria katika kituo hicho
kilichopo chuo cha elimu ndani ya UDOM Dodoma.
Madereva wa Bodaboda wakiwa
wamekusanyika pamoja wakijadiliana jambo wakati wakifikili nini cha kufanya
baada ya kuona askari walinzi wa
chuo kikuu cha Dodoma [ UDOM] Kuwafukuza na kuwataka kutopakilia
Abiria katika kituo hicho kilichopo katika majengo ya mchepuo wa
elimu.
Waendesha pikipiki za
kusafirishia abiria maarufu kama Bodaboda wakuwa
wameziegesha katika kituo cha Daladala cha maktaba ya ualimu
kilichopo Chuo kikuu kikuu cha Dodoma [UDO], madereva hao
wamelalamikia kunyanyaswa na walinzi chuoni hapo kwa kukamatwa na
kutishiwa kuvunjwa miguu bila sababu za kueleweka.