Habari
zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka Mahakama Kuu, zinasema kuwa
Mahakama Kuu imeahirisha hukumu ya Zitto Kabwe dhidi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambayo ilikuwa imepangwa kutolewa leo
asubuhi.
Kwa
maamuzi hayo ya Mahakama ya kuahirisha hukumu, yalionekana kuwakera
pande zote mbili wafuasi wa Zitto na viongozi wengine wa Chadema.
Kwa
mujibu wa taarifa za awali kwa watu waliokuwa mahakamani hapo, kesi
hiyo sasa hukumu yake itasomwa kesho saa nane mchana. Kesi hiyo ni
mwendelezo wa mgogoro mkubwa wa ulio ndani ya Chadema dhidi ya Kabwe
anayedai kuwa hiyo ni vita ya ukombozi dhidi ya wahafidhina kwenye chama
chao.
Jana katika mitandao ya kijamii walikuwa wakirushiana makombora ambapo Zitto alionekana kumjibu Tundu Lissu kama ifuatavyo.
"Lissu
anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono.
Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe
tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.
Nadhani
alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007)
Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema
kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka
2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.
Pia
hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni.
Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za
chama kutoka Conservative Party?
Nimefanya
internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya
mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri
Mkuu Pinda.
Lissu
awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni
kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia
deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club
Bilicanas.
They
must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi
kuheshimu mke wake aliyemzaliwa mtoto hawezi kunmyooshea mtu kidole
kuhusu maadili.
No comments:
Post a Comment