Wednesday, January 22, 2014

MAFURIKO YAVUNJA DARAJA DUMILA MAGARI KUTOKA DODOMA NA DAR HAYAVUKI.


MAFURIKO YAVUNJA DARAJA LA BEREGA
Mafuriko yamevunja daraja la Berega ambapo maji yanapita juu ya daraja lingine la Dumila katika barabara ya Morogoro – Dodoma hali iliyosababisha wasafiri kuendelea na safari zao. Hali hiyo inasababisha magari kupita upande mmoja kwa shida na wengine kusitisha safari zao na kugeuza huku kukiwa na msururu mkubwa wa magari yanayosubiri hali hiyo itengamae, watu walioshuhudia hali hiyo wamesema mafuriko hayo imetokana na mvua kubwa iliyonyesha maeneo hayo ambayo haijawahi kutokea kwa siku za karibuni na kutiririsha maji mengi kiasi hicho

MH:MBUNGE WA CHALINZE SAID RAMADHANI BWANAMDOGO AFARIKI DUNIA.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (Mb), anasikitika kutoa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Saidi Ramadhani Bwanamdogo Kilichotokea leo Jumatano asubuhi tarehe 22.1.2014 Katika hospitali ya MOI DSM alipokuwa amelazwa kwa Matibabu. 
Ofisi inaendelea na taratibu za mazishi 
kwa kushirikiana na familia ya Marehemu.
Inna llilah Waina Illaih Rajiun!

SPIKA WA BUNGE,
22.01.2014

Sunday, January 19, 2014

NEWS ALERT:RAIS ATANGAZA RASMI MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI:

UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
______________________________ ________________


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-

1. OFISI YA RAIS


Hakuna mabadiliko.

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS


2.1 Waziri wa Nchi (Muungano) - Hakuna mabadiliko

Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)

Waziri wa Nchi (Mazingira).

Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)

Naibu Waziri


3. OFISI YA WAZIRI MKUU


Hakuna mabadiliko

4.0 WIZARA

4.1 WIZARA YA FEDHA

Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)

Waziri wa Fedha

Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)

Naibu Waziri wa Fedha (Sera)

Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)

Naibu Waziri wa Fedha


4.2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


Hakuna mabadiliko


4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

4.3.1 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
Waziri wa Katiba na Sheria

Naibu Waziri - Hakuna mabadiliko


4.4 WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Hakuna mabadiliko


4.5 WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

4.5.1 Waziri - Hakuna mabadiliko

4.5.2 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara


4.6 WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa


4.7 WIZARA YA UJENZI


Hakuna mabadiliko

4.8 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

4.8.1 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani

Naibu Waziri - Hakuna Mabadiliko



4.9 WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii


4.10 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

4.10.1 Waziri: Hakuna mabadiliko

4.10.2 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi


4.11 WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

4.11.1 Waziri: Hakuna mabadiliko

4. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto


4.12 WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

4.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi


4.13 WIZARA YA KAZI NA AJIRA


Hakuna mabadiliko

4.14 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


Hakuna mabadiliko

4.15 WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

4.15.1 Waziri - Hakuna mabadiliko

4.15.2 Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi


4.16 WIZARA YA MAJI

4.16.1 Waziri - Hakuna mabadiliko

4.16.2 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji


4.17 WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

4.17.1 Waziri - Hakuna mabadiliko

4.17.2 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika


4.18 WIZARA YA UCHUKUZI

Hakuna mabadiliko


4.19 WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

4.19.1 Waziri - Hakuna mabadiliko

4.19.2 Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo


4.20 WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii

4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

4.21 WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri - Hakuna mabadiliko


Naibu Waziri (Madini) - Hakuna mabadiliko


4.21.3 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)

Naibu Waziri (Nishati)



Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI


Ikulu
DAR ES SALAAM

19 Januari, 2014

Saturday, January 11, 2014

ABIRIA WA TRENI WALIOKWAMA DODOMA WAZIDI KUTESEKA HUKU SAFARI YAO IKIWA BADO NI KITENDAWILI.

Abiria waliokwa na treni Dodoma wakusubili mabasi kwa ajili ya usafiri
wa kuelekea mikoa ya Morogolo na Dar es saalam ambapo shirika la Reli
limewakodia mabasi kutokana na kushindwa kuendelea na safari kutokana
na Mafiriko Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa Dodoma.

Abiria hao wakiwa hawajui la kufanya kutokana na kukosa chakula katika
stesheni ya rellwe Dodoma walipotangaziwa kuanza kusafirishwa kwa
mabasi laki mpaka kufikia jana jioni zaidi ya abiria 900 walikuwa bado
hawapatiwa usafiri huo.

mizigo ya abiria hao ikiwa imetapakaa huku wakiwa bado hawajui hatma yao ya safari.
PICHA NA JOHN BANDA DODOMA

WAKUU WA IDARA MBALIMBALI WILAYANI KONDOA WAPEWA MTIHANI MAALUMU WA KUPIMA UWEZO WAO KATIKA KUFUATILIA MASUALA YA WANANCHI.

Wakuu wa idara mbalimbali wilayani kondoa wakijitahidi kujibu mtihani uliotolewa Jana na mkuu wa mkoa wa dodoma (hayupo pichani) wenye lengo la kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wa viongozi ngazi mbalimbali wilayani kondoa kuanzia watendaji kata, maafisa tarafa Wakuu wa idara mpaka mkuu wa wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya kondoa Omary Kwaangw' (kulia) akiumiza kichwa kutafuta majibu ya mtihani uliotolewa na mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema nchimbi (watatu kutoka kulia) ill kupima kiwango cha ufuatiliaji wa mambo na utendaji wa viongozi wa wilayani kondoa.zoezi hili litafanyika kwenye wilaya ya zote za mkoa wa dodoma
Mbunge wa kondoa kaskazini Mhe Zabein Mhita akichangia hoja juu ya tathimini ya ufuatiliaji wa mambo na  utendaji wa viongozi na watendaji  wa serikali wilayani kondoa jana, katikati ni katibu tawala msaidizi anayeshughulikia serikali za mitaa Dodoma Ndg. Emanuel kuboja na kulia ni mkuu wa mkoa wa dodoma Dr Rehema nchimbi.