
Friday, April 14, 2017
MAUAJI YA KUTISHA MKOANI PWANI ,MAJAMBAZI YAUA POLISI 7.OPARATION YA KUWASAKA WAUAJI YAANZA.

picha za baadhi ya askari waliouwawa



Na Mathias Canal, Dar es salaam
Askari wa jeshi la Polisi Mkoani Pwani Jana waliwaua watu wanne
watuhumiwa katika majibizano ya risasi Mara baada ya kutokea Mauaji ya
Askari nane waliokuwa wanatoka kubadilishana Rindo katika Barabara ya
Dar es salaam- Lindi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo
(CP) Nsato Marijani Mssanzya wakati wa mkutano wake na waandishi wa
Habari alisema kuwa
Jana tarehe 13/04/2017 majira ya saa kumi na mbili na robo jioni maeneo
ya Mkengeni, Kata ya Mjawa, Wilaya ya Kibiti, Mkoani Pwani, Majambazi
ambao idadi yao haijafahamika wakiwa na silaha za Moto walishambulia kwa
risasi gari la Polisi lenye namba PT 3713 Toyota Land Cruiser na kuwaua
askari hao nane.
Kamishna Mssanzya amewataja askari waliouwawa katika tukio hilo kuwa ni
A/INSP Peter Kigugu, F.3451CPL Fransis, F.6990PC Haruna, G.3247 PC
Jackson, H.1872 PC Zacharia, H.5503 PC Siwale, H.7629 PC Maswi na H.7680
PC Ayoub.
Kamishna Mssanzya alisema kuwa katika tukio hilo majambazi hayo yalipora silaha saba zikiwemo SMG Nne na Long Range Tatu.
Ameeleza kuwa Mara baada ya tukio hilo hatua za Kiintelijensia na
kiupelelezi zilichukuliwa na zilipelekea askari kufuatilia na kubaini
maficho ya muda ya majambazi hao na katika majibizano ya risasi
majambazi wanne waliuawa na bunduki nne kupatikana, Mbili zikiwa ni zile
zilizoibiwa katika tukio la Mkengeni na bunduki mbili zikiwa Mali ya
majambazi hayo.
Kamishina Mssanzya amewasihi wananchi wakati Jeshi la Polisi likiendelea
kuwatafuta majambazi hao wao kuendelea kuwa watulivu na kuendelee kutoa
taarifa kwa jeshi la Polisi zitakazosaidia ukamataji wa wahalifu hao
Tuesday, April 11, 2017
KIKAO CHA MAJADILIANO BAINA YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI MJINI DODOMA.
Waziri wa fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa
TPSF Dkt. Reginald Mengi pamoja na makamu mwenyekiti TPSF Mr. Salum
Shamte.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, (mwenye suti
nyeusi), kushoto ni Mhe. Dkt), Philip Mpango Waziri wa fedha na Mipango,
Dkt. Reginald Mengi Mwenyekiti TPSF, pamoja na Ndugu Salum Shamte
Makamu mwenyekiti TPSF
Baadhi ya washiriki wa Kikao cha majadiliano baina ya serikali na sekta binafsi.
Friday, March 31, 2017
WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE.DKT. MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga
ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimpigia makofi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam
Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa
mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka
kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili
yake.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua
Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es
Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza
mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn
aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia
jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn
akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya
mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John
Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu
jijini Dar es Salaam.

Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri
Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn
akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal
One jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
Wednesday, March 29, 2017
RC MAKONDA AWEKWA KITI MOTO BUNGENI DODOMA.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akihojiwa Leo mbele ya kamati ya bunge
Na Ofisi ya bunge, Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda leo amehojiwa na Kamati
ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusiana na tuhuma za
kuingilia haki, uhuru na madaraka ya Bunge.
Mhe. Makonda aliwasili Bungeni Dodoma majira ya saa nne asubuhi
kuitikia wito wa Kamati hiyo uliotokana na Azimio la Bunge lililotolewa
na Bunge, Februari 8, 2017 katika Kikao cha Nane cha Mkutano wa Sita
wa Bunge ambapo amehojiwa na kamati hiyo kwa muda wa masaa matatu kuhusu
tuhuma zinazomkabili.
Katika kikao hicho, Bunge liliazimia kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mhe. Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti
kuitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge
baada ya Bunge ili kujibu tuhuma hizo.
Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kumaliza kazi yake, Mwenyekiti wa
Kamati ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. George
Mkuchika alisema Kamati hiyo imekutana leo baada ya kuagizwa na
Mheshimiwa Spika wa Bunge kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge.
“Tumefanya kikao hiki cha Kamati baada ya kuagizwa na Mhe. Spika kwa
kuwa kwa Mujibu wa Kanuni zetu, Kamati hii inakutana pale tu inapoagizwa
na Spika wa Bunge,” alisema.
Alisema Mhe. Spika aliiagiza Kamati hiyo imuite Mhe. Makonda mbele ya
Kamati kufuatia azimio hilo la Bunge lililopitishwa na Bunge Februari
8, ambapo pamoja na mambo mengine Mkuu huyo wa Mkoa alitakiwa kufika
mbele ya Kamati kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Alisema kwa mujibu wa Azimio hilo, Mhe. Makonda alidaiwa kutoa kauli
kupitia Televisheni ya Clouds akidai kwamba wabunge wanasinzia Bungeni
jambo lililoonekana kwamba ni kudharau Bunge.
“Napenda kutoa taarifa kwamba Mhe. Makonda leo amekuja mbele ya Kamati
na ametupa ushirikiano mzuri, tumepokea maelezo yake na Kamati imemaliza
kazi yake,” alisema.
Alisema kama ilivyo utaratibu, Kamati yake itakabidhi taarifa yake kwa
Mhe. Spika kwa mujibu wa Kanuni ambapo Spika ndiye atakaeamua namna ya
kutoa raarifa kuhusu kazi ya Kamati hiyo.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)
