Sunday, March 23, 2014

WATU WASIOJULIKANA WAVAMIA KANISA NA KUWAMIMINIA RISASI WAUMINI NA KUUA HUKO MOMBASA NCHINI KENYA

                            mkuu wa jeshi la polisi kenya (I G P)david kimaiyo.
polisi nchini kenya wamesema watu wenye silaha wamewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili baada ya kuvamia kanisa wakati wakiwa kwenye ibada ya jumapili na kuwamiminia risasi waumi hao huko mombasa

polisi wa kituo wilaya ya likoni huko mombasa  robert mureithi amesema kuwa watu hao wamemuua mwanaume mmoja na mwanamke mmoja katika tukio hilo ambalo watu kumi wamejeruhiwa,huku kukiwepo kwa onyo la waislamu kushambulia maeneo kadhaa.

Friday, March 21, 2014

RAIS KIKWETE AHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA NA KULIFUNGUA RASMI.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mjini Dodoma leo 
Rais Kikwete akisisitiza jambo wakati akilihutubia Bunge la Maalum la Katiba Tanzania.
Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakifuatilia hutuba ya Rais Kikwete wakati akilihutubia bunge la Maalum la Katiba Mjini Dodoma leo jioni.


Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Tanzania wakimsikiliza Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia bunge hilo. 
Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao Nchini Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais Dkt Jakaya Kikwete, wakati akihutubia Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma leo jioni.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akilihutubia Bunge hilo leo jioni Mjini Dodoma.

Wednesday, March 19, 2014

CCM WAZINDUA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA CHALINZE

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Uwanja wa  Miembesaba, Chalinze mkoa wa Pwani.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakiwapungia mkono wananchi wa Jimbo la Chalinze na WanaCCM waliofika kwa wingi kwenye Uzinduzi wa Kampeni za CCM,zilizofanyika leo Machi 19, 2014 kwenye Viwanja vya Polisi Chalinze,Mkoani Pwani.
Mjumbe wa NEC na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akijumuina na WanaCCM wa Jimbo la Chalinze huku akiwa amebeba bango la Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete.

Monday, March 17, 2014

BREAKING NEWZ:MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH WARIOBA ASHINDWA KUWASILISHA RASIMU YA KATIBA BUNGENI WABUNGE WAZOMEA BUNGE LA AHIRISHWA.


Katika hali isiyotarajiwa na wengi Wabunge wa Bunge maalum la katiba wamezomea jioni yaleo na kusababisha bunge maalumu la katiba kuhairishwa pale aliyekuwa Mwenyekiti wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi jaji Warioba kufika jioni ya leo nakutaka kuwasilisha rasimu ya katiba;iliyopelekea mwenyekiti wa bunge hilo Mh Sita kuhairisha bunge hilo baada ya yeye kushindwa kutumia njia ya kumfanya jaji Warioba kuendelea kuwasilisha rasimu hiyo. MUNGU SAIDIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUPATE KATIBA MPYA

GODFREY MGIMWA AIBUKA KIDEDEA KWA USHINDI WA KISHINDO JIMBO LA KALENGA MKOANI IRINGA.


Godfrey Mgimwa akibebwa juu juu na wanachama na wapenzi wa CCM baada ya matokeo kuonyesha ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga leo.
Mashabiki wa CCM wakimwayamwaya kwa furaha baada ya kupata matokeo hayo ya awali.
*************************************
MATOKEO YA AWALI
Mpaka sasa CCM inaongoza katika kata 11 kati ya 13 
TOSA no.1 CCM 98 ,Chadema 20, CHAUSTA 0
 
Ipamba no2. CCM 104, Chadema 10,CHAUSTA 0
Isakulilo CCM 83,Chadema 8,CHAUSTA 0
 

Kilindi A CCM 69 ,Chadema 23, CHAUSTA 0
Ofisi ya Kijiji(Kilindi) CCM 117, Chadema 53, CHAUSTA0
 
Zahanati  CCM 117,Chadema 67, CHAUSTA 1

Ifunda
Kivalali A CCM 99 Chadema 19 CHAUSTA 0
 
Kivalali B CCM 109 Chadema 14, CHAUSTA 1
Muwimbi CCM164, Chadema 22 CHAUSTA 0
 

Mahanzi CCM 130 Chadema 46 CHAUSTA 0
Ikungwe A CCmM 131 Chadema 23 CHAUSTA 0
 
Ikungwe B CCM 216 Chadema 13 CHAUSTA 0
Magunga CCM 184 ,Cadema 4 CHAUSTA1
 
Wasa CCM 149,Chadema 15 CHAUSTA 0
Usengelidete CCM 260,Chadema 46,CHAUSTA O

Monday, March 10, 2014

AL-AHL CHUPUCHUPU WATOKEA KWENYE TUNDU LA SINDANO KWAO-ILA YANGA KIBOKO YAO.


Mchezo wa raundi ya pili wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya wenyeji Al Ahly imemalizika usiku huu, huku 
Mabingwa hao wa Afrika wakitokea kwenye tundu la sindano baada ya kupata ushindi wa penati 4-3.

Katika mikwaju ya penati, Mabeki Mbuyu Twite na Oscar Joshua walikosa baada ya penalti zao kupanguliwa.

Kipa Deo Munishi aliswazisha makosa yao baada ya kupangua penalti 2.  Ilikuwa ni zamu ya Said Bahanuzi ambaye kama angefunga, basi Yanga ingefuzu.

Lakini mkwaju aliopiga ulitoka nje na baada ya hapo, Ahly wakamalizia penati moja na kufuzu kwenye hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa hisani ya Salehjembe

Friday, March 7, 2014

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LATAJA MAJINA YA MAKAHABA SUGU DODOMA NA KUAHIDI KUWASAKA.



Na.Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea kufanya msako katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata wanawake wapatao 15 wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao kutoka mikoa mbalimbali nchini. Msako huo ulifanyika tarehe 05/02/2014 majira ya 21:00hrs katika mitaa ya uhindini na Air Port.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME - SACP amewataja watu hao kuwa ni:

1.   VERONICA D/O JOEL mwenye miaka 23, Mnyakyusa mkazi wa Sai Mbeya.

2.   ROSE D/O MICHAEL mwenye miaka 30, Mgogo, Mkazi wa Kikuyu Dodoma.

3.   MARIAM D/O JORDAN mwenye miaka 26, Mhehe mkazi wa Tukuyu Mbeya.

4.   REHEMA D/O RAMANDANI mwenye miaka 38, Mlugulu makazi wa Airport Morogoro.

5.   JOYCE D/O MARTINE mwenye miaka 22, Mnyamwezi mkazi wa Chinangali West Dodoma.

6.   FATIA D/O SARATIELI mwenye miaka 20, Mgogo mkazi wa Makanda Bahi Dodoma.

7.   BOKE D/O CHACHA mwenye miaka 27, Mkurya mkazi wa Tarime Mara.

8.   SWAUMU D/O BAKARI mwenye miaka 23, Mnyamwezi mkazi Chinangali Dodoma.

9.   ROSS D/O MASAKI mwenye miaka 28, Mchaga mkazi wa Sanya juu Moshi.

10.               SCOLASTIA D/O COSTANTINO mwenye miaka 22, Mnyakyusa mkazi wa Gongolamboto Dar es salaam.

11.               HAPPY D/O JULIUS mwenye miaka 31, Mnyamwezi mkazi wa  Urambo Tabora.

12.               AISHA D/O HASSAN mwenye miaka 38, Mbulu mkazi wa Babati Manyara.

13.               JULIANA D/O DOMINICK Mwenye miaka 31, Mnyakyusa, mkazi wa Airport Dodoma.

14.               DATIVA D/O LUKWEMBE mwenye miaka 29, Mhaya mkazi wa Kiziba Bukoba Kagera.

15.               DORIN D/O MASSAWE mwenye miaka 23, Mchaga mkazi wa Kiboshomaro Moshi.

Aidha Kamanda MISIME amesema katika msako huo watu wawili wanaume walikamatwa wakiwa na mirungi robo kilo katika mtaa wa barabara ya nane (8) Manispaa ya Dodoma ambao ni NASSOR S/O ALLY mwenye miaka 45, Mwarabu mkazi wa barabara ya kumi na AYUBU S/O TEPO mwenye miaka 40, Muarusha, Fundi cherehani mkazi wa Chamwino.

Pia huko katika Wilaya ya Kongwa kijiji cha Mlanje kata ya Matongoro Tarafa ya Zoisa alikamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SHEDRACK S/O MACHILE mwenye miaka 46, Mgogo, Mkulima akiwa na Lita 30 za pombe ya moshi akiziuza.

Kamanda MISIME amesema msako unaendelea na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.