Saturday, February 15, 2014

IGP MSTAAFU SAID MWEMA AAGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM.


 IGP Mstaafu Said Mwema akiwa katika Gari Maalum la wazi huku akipunga mikono kwa Maafisa, Askari, Wageni Waalikwa na Wananchi mbalimbali katika hafla fupi iliyofana sana ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma. Sherehe hizo zimefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
 IGP Mstaafu Said Mwema(kushoto) akimkabidhi kitara IGP Mpya wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu(kulia) ikiwa ni ishara ya Makabidhiano ya Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Polisi hapa Nchini. Sherehe hizo zilizopambwa na Gwaride Maalum lililounndwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi imefana sana katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
 Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakipunga mikono wakati IGP Mstaafu, Said Mwema(hayupo pichani) akipita katika Gari Maalum la wazi. Hafla hiyo fupi imefanyika kwa ajili ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma(wa Nne toka kulia) ni Mkrugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid(tatu toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile).
 IGP Mstaafu, Said Mwema akipokea Salaam ya heshima na utii iliyotolewa na Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi(hawapo pichani) katika hafla fupi ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 15, 2014 katika Viwanja vya Polisi barracks Jijini Dar es Salaam.
 IGP Mstaafu, Said Mwema akikagua Gwaride Maalum alililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria.

CCM WATAKIWA KUTOKUWA WANYONGE DHIDI YA VURUGU ZA CHADEMA NYAKATI ZA UCHAGUZI-JK.


MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewapa rungu wana-CCM akiwataka  kuacha kujifanya wanyonge dhidi ya vitendo vya fujo ambavyo hufanyiwa na  Chadema nyakati za uchaguzi.

Rais Kikwete amesema hayo leo, wakati akiongoza kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma.

"Uchaguzi wa Kalenga ndiyo huo upo mbele yetu, hadi sasa hakuna tatizo lililojitokeza kama Arumeru mambo yapo shwari kabisa, lakini tujue tu kwamba pale tunaenda kushindana na watu (Chadema) ambao wao silaha yao ya kwanza ni vujo.. ninaagiza sasa lazima wana CCM kukabiliana na fujo zao. Unyonge basi.", alisema Rais Kikwete na kuongfeza;

"CCM kuendelea kujifanya wanyonge kila mara sasa basi. Haiwezekazi watu wanafanya vujo hadi kuwatoboa watu macho ninyi nmanyongea tu, hili haliwezekani. Tazama pale Ingunga  mtu wenu alimwagiwa tindikali hali leo ana  ulemavu wa kudumu kisa uchaguzi tu, aah haiwezekani kabisa", alisema Rais Kikwete.

Mapema Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete alipongeza wana CCM na viongozi wao katika Kata zote zilizofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani na hatimaye CCM kuibuka na ushindi wa Kata 23, Chadema ikiambulia tatu na NCCR Mageuzi kimoja.

Hata hivyo Rais Kikwete alisema, licha ya CCM kuzoa kata nyingi kwenye uchaguzi huo, viti vinne kwenda kwa upinzani bado ni doa hivyo lazima CCM ihakikishe inazikomboa kata hizo nyakati za chaguzi zijazo.

"Ni kweli tumezoa kata nyingi, lakini kwa kuwa lengo letu CCM kila wakati ni kushinda tu, hatua hiyo ya kuzikosa kata nne bado ni doa lazima kuzikomboa kata hizo chaguzi zijazo", alisema, Rais Kikwete.

Pia alipongeza CCM, kwa ushindi iliopata kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Kimbesamaki na kwamba CCM inaona fahari kulirejesha jimbo hilo mikononi mwake, kwa kuwa ilikuwa imelazimika kumfuza mwakilishi wake wa awali kwenye jimbo hilo kwa kuwa alikuwa msaliti aiyefaa kuendelea kuwemo ndani ya Chama

Friday, February 14, 2014

STEPHEN WASIRA NAYE AHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI YA CCM MJINI DODOMA.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Ndugu Stephen Wassira akitoka nje ya ukumbi wa White House baada ya kumaliza mahojiano na Kamati Ndogo ya Maadili.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Ndugu Stephen Wassira akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi,Wassira aliwaeleza waandishi kuwa hakukuwa na tuhuma juu yake.
.

BANK YA ACB DODOMA YAWEZESHA MAFUNZO YA UJASILIA MALI KWA WAJASILIA MALI ZAIDI YA 1000 YALIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA POLISI JAMII DODOMA.


Wajasiriamali mkoani Dodoma wakishangilia jambo walipokuwa katika
ukumbi  wa polisi jamii walipokuwa kwenye mafunzo ya utengenezaji wa
vitu mbalimbali kwa kutumia mikono, ikiwemo Batiki, keki, ubuyu, krips
na usindikaji wa vyakula na matunda yaliyoandaliwa na Kampuni ya
Wajasriliamali kwanza Entarprises ya jijini Dar es laam na kudhaminiwa
na Benk ya wajasriamali Tanzania [ACB]
Mkurugenzi wa kampuni ya Wajasiriamali kwanza DKT Didas Lunyungu
akifafanua jambo wakati alipokuwa azunguza na wajasiriamali wa mkoa wa
Dodoma walioshirikai mafunzo ya utengenezaji na usindikaji wa bidhaa
mbalimbali yaliyofanyika kwa siku 4.
Meneja wa kampuni hiyo Saravai Izinah akimtamburisha Meneja  masoko wa benki ya wajasiriamali Tanzania Inocent Ishengoma [ACB] ambao ndiyo
waliokuwa wadhamini wakuu wa mafunzo hayo yaliyodumu kwa kwa sik4 nakujumuisha wajasiriamali 1000 walishiriki wa mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DKT Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya amoja na wafanyakazi wa kampuni ya wajasiriamali kwanza waliokuwapokuwa wakiwafundisha wajasiriamali wa Dodoma namna ya kutengenezana kusindika bidhaa mbalimbali.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma DKT Rehema Chimbi akizungumza na wajasiriamali wa mkoa huo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya siku 4 yaliendeshwa na Kampuni ya wajasiriamali kwanza kwa udhamini wa  Benki ya akiba[ACB].
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DKT Rehema Nchimbi akimkabidhi meneja msaidizi wa benki ya wajasiriamali Tawi la Dodoma Christine Wachona cheti cha ushiriki wa mafunzo ya wajasiriamali ambao pia walikuwa wadhamini wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 4.

PICHA NA JOHN BANDA