Friday, September 27, 2013

BABU WA KIKOMBE AMBILIKILE MWASAPILA ANA KWA ANA NA WAZIRI MKUU LOLIONDO .


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisaliiana na Ambilikile Mwasapila maarufu kwa jina la Babu  wakati alipopita katika kijiji cha Samunge akilelekea Digodigo kuhutubia mkutano wa hadhara Septemba 24, 2013. Alikuwa katika  ziara ya wilaya  ya Ngorongoro

Wednesday, September 25, 2013

PICHA ZA KIKOSI MAALUM CHA JESHI LA KENYA KATIKA HARAKATI ZA KUPAMBANA NA MAGAIDI HUKO WESTGATE,JUMLA YA WATU 72 WAMEPOTEZA MAISHA WAKIWEMO ASKARI 6 NA MAGAIDI 5.

Hapa ni mwendo wa mjusi 
Mawasiliano yakiendelea
Licha ya kadhia iliyopo hapo lakini Vibaka walikuwa wakinyemelea na hapa Polisi waliwapiga Bomu la machozi kuwatawanya.
Wazee wa kazi wakipata Chai

HUYU NDIYE MSICHANA WA KIZUNGU ANAYEDAIWA KUONGOZA MAUAWAJI WESTGATE NAIROBI KENYA


Wakati mapambano bado yanaendelea dhidi ya wanamgambo wachache wa al Shabaab waliobaki ndani ya Westgate Mall, maofisa wa Kenya wamesema angalau al Shabaab watatu wameuawa katika harakati za kuokoa mateka
Taarifa zinasema mmoja wa magaidi hao ni mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa mwanamke huyo aliyetajwa ni Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White Widow” au “Mjane Mweupe” au “Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha anaripotiwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mume wa Samantha alikua mpiga mabomu wa kujitoa mhanga (suicide bomber) anayeitwa Germaine Lindsay ambaye baada ya kusilimu alitumia jina la Abdullah Shaheed Jamal.
Abdullah Jamal alikua ni mmoja wa magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga mabomu ya kujitoa mhanga katika treni tatu na kuua watu 56 nchini uingereza Julai 7, 2005 ambao unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7

Tuesday, September 24, 2013

AJALI MBAYA SANA DODOMA, BASI LA AL-SAYD LAGONGANA USO KWA USO NA LORI NA KUUA WATU 6 PAPO HAPO

 
Na John Banda, Dodoma
MWENDO kasi wa speed 140 aliyokuwa akiutumia Dereva wa Basi la Al sayd Expess umesabisha vifo vya zaidi ya watu 6 akiwemo yeye na dereva wa lori alilogongana nalo na wengine 17 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa .
Ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha chinangali 2  wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati basi hilo lenye namba za usajili T 433 DLR  lililokuwa likitokea Dar es saam  kuja mkoani hapa lilipogongana uso kwa uso na lori hilo lenye namba za usajili T102 CGR aina ya Layland Daf lilikuwa na tera.
moja wa majeruhi wa ajali hiyo Juma Yusuph 31 mhehe  mkazi wa Chidachi manispaa ya Dodoma alisema mwendo huo ulibadilika na kuwa mkubwa kuanzi walipotoka mkaoni Morogoro kiasi cha kufikia kasi hiyo.
‘’Mimi nilikuwa nimekaa mbele karibu na dereva nilipochungulia nikaona  speed inasoma 140 huku jamaa akiyapita magali ya mizigo zaidi ya 4 kwa pamoja kama unavyoona mimi nimevunjika mguu lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa Yule dereva ni kama alipanga kujiua na kweli nilishuhudia baadhi ya viungo vyake mbele ya lori’’, alisema yusuph.
Majeruhi wa ajali hiyo ambao wengi wao walivunjika viungo vikiwemo miguu na mikono walisema mwendo mkubwa uloanza baada ya kutoka  Morogoro
Kaimu kamanda wa polisi mkoa Damas Nyanda aliwataja majina waliopoteza maisha mbele ya  wandishi wa habari kuwa Dereva wa lori Hassan Mohamed umri kati ya 30,35, Ahmed Said, Husen Rajab, Imran Sharif wakazi wa Dar, na Dereva wa Basi hilo Nizar Akran Khan mkazi wa Mpwapwa  wakati mwili wa marehemu mmoja bado haujatambuliwa.
Kaimu kamanda huyo alisema Alisema Miili ya maremu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma na wengine 17 waliojeruhiwa kulazwa wakiwemo 7 wanawake na wanaume 10
Nyanda  alisema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2.30 usiku wa juzi  jumapili  ni Mwendo kasi wa Dereva wa Basi hilo ambapo ashindwa kulimudu wakati akijaribu kusimama ili kujaribu  kujiepusha na ajali hiyo.
Jeshi hilo la polisilimetoa wito kwa watumiaji wa barabara kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani huku wakiwa natahadhali ya kujua kuwa kuna watumiaji wengine.
 

Daktari wa Mifipa wa hospital ya Rufaa ya Dodoma Maitundo Stanley akimhudumia mmoja wa majeruhi  wa ajali iliyohusisha Basi la Al sayed lililokuwa likitoka Dar es  laam kwenda Dodoma na Lori la mizigo uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 6.

 
Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Damas Nyanda akitoa ufafanuzi kuhusu ajali iliyohusisha basi la Al sayed na Lori la mizigo na kusababisha vifo vya watu 6 na wengine 17 kujeruhiwa vibaya ikiwemo kuvunjika viungo mbalimbali vya miili yao.

Askari wa kikosi cha usalama Barabarani akichukua maelezo kwa mmoja wa majeruhi wa basi la al sayd express lenye namba za usajili T433 BLR lililogangana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mahindi kupeleka Dar es salaam.

Sunday, September 22, 2013

HAPPYNESS WATIMANYWA KUTOKA DODOMA ATWAA TAJI LA REDDS MISS TANZANIA 2013.

 redds miss tanzania 2013 HAPPYNESS WATIMANYWA akipunga mkono mara baada ya ktangazwa kuwa mshindi wa taji hilo kwa mwaka huu,kushoto ni mshindi namba 2 LATIFAH MOHMED na kulia ni mshindi namba 3 CLARA BAYO.
 warembo wa redds miss tanzania 2013 wakiwa jukwaani katika onyesho liliofanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY jijini dar es salaam
 warembo wakiwa wamependeza sana
warembo wakiwa katika shoo ya pamoja

SAFARI HII DODOMA FAMILY YATUA BABATI HAPA MKOANI MANYARA.

Sagulasagula ya nguo ikiendelea, wateja wakijinunulia  nguo kwa bei  poa kabisa moja ya magulio makubwa yaliyopo sehemu ya MAGUGU -BABATI.
Kama ilivyokuwa kawaida kwenye minada/magulio ya aina hii  kitu cha nyama choma hakikosekani, hapa bwana jerry mwakyoma mkuu wa msafara alivyobambwa na camera yetu akingojea nyama ziive.




Wadau hawa walikutwa na canera yetu wakitafuna nyama choma kwenye moja la banda la mamalishe ama mama pima kama wanavyojulikana kwenye baadhi ya