Monday, August 26, 2013

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA CHINI YA MWENYEKITI RAIS JAKAYA KIKWETE KIKIENDELEA.


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo, Agosti 25, 2013. Kikao hicho kilifanyika kwa ajili ya kukutana Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Constansia Buhiye,  Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Abedi Mushi, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba mjini na Meya wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani, kuhusu mgogoro wa madiwani wanane wa CCM Manispaa ya Bukoba. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constansia Muhiye na Katibu wa CCM wa mkoa huo, Abedi Mushi wakisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati kuu mjini Dodoma leo.
 Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki akisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati Kuu ya CCM Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimsikiliza kwa makini Mwana-CCM mwenye ulemavu wa miguu, Shija Luhende kutoka Mwanza, ambaye alimkuta kwenye viwanja vya Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma leo, akitafuta msaada wa baiskeli. 
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,  Abdallah Bulembo akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jenista Mhagama, nje ya ukumbi, Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma

Saturday, August 24, 2013

MWENYEKITI WA CCM TAIFA MH JAKAYA KIKWETE AWASILI DODOMA TAYARI KWA KUONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliofika uwanjani kumlaki.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Adam Kimbisa.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Khamis Sadifa Juma.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtumishi wa Chama Cha Mapinduzi  ndugu Octavian Kimario .


mkereketwa na mhamasishaji mkuu wa ccm mkoa wa dodoma bi bushura kitwana akimlaki mh rais jakaya kikwete alipowasili katika uwanja wa ndege mkoa wa dodoma tayari kwa kuongoza vikao vya chama hicho.

MWENGE WA UHURU WAHITIMISHA MBIO ZAKE MKOANI DODOMA TAREHE 22/8/2013.

Viongozi/timu ya Mkoa wa Morogoro wakiusubiri kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Dodoma Tayari kwa kuukimbiza Mkoani Morogoro kwa kuanzia na Wilaya ya Gairo.


kutoka kuishangilia yanga mpaka kukimbiza mwenge/Vijana wa Kikundi cha hamasa kutoka Dodoma wakishangilia wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya Mkoa wa Dodoma na Morogoro yaliyofanyika kwenye kijiji cha ukwamani majawanga Kongwa kilichopo mpakani mwa Mikoa hiyo miwili.
 Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera kwa ajili ya kuukimbiza Mkoani humo.


Friday, August 23, 2013

RAIS MUGABE AAPISHWA RASMI MJINI HARARE.


 Rais wa Zimbabwe Mhe Robert Gabriel Mugabe akila kiapo katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa kwake jana Agosti 22, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoka katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini zimbabwe, Mhe Adadi Rajabu.
 Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakimpongeza Rais Robert Mugabe katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa rais huyo

Thursday, August 22, 2013

KAMATI KUU YA CCM YATOA RATIBA YA VIKAO VYAO KUANZIA KESHO MJINI DODOMA.


Kamati Kuu ya CCM Taifa itakutana tarehe 23.8.2013 ikifuatiwa na Halmashauri Kuu keshokutwa asubuhi  ambapo itakuwa kwa siku mbili.

Ajenda Kuu ya Kamati Kuu itakuwa  kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa White House,Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Pia Kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala ya Utumishi.

Alisema siku ya Jumamosi asubuhi tarehe 24,kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri.
Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.

GURUMO ATANGAZA KUSTAAFU MUZIKI RASMI.


Mwnamuziki mkongwe wa muziki wa dansi wa bendi ya Msondo Ngoma, Mzee Muhidin Gurumo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake wa kustaafu rasmi kazi ya muziki aliyoifanya kwa muda wa miaka 53 sasa. Gurumo alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. 
 
MWANAMUZIKI mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.

“Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu,”alisema  Mzee Gurumo.
Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo alisema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake.

 “Mimi  nimeimba kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli sina,”alisema Mzee Ngurumo. Hata hivyo alisema  nashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.

Vilevile Mzee Gurumo amewaasa vijana kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani kwani ndio chimbuko la bongofleva na kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa wavumilivu kukaa muda mrefu kwenye bendi moja ili hata wanapoondoka mchango wao uthaminiwe.

 Mzee   Gurumo  ambaye ana mke na watoto wanne alisema kuwa katika maisha yake ya muziki alifanikiwa kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki Hussein Jumbe na Hassani Lehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya anavutiwa na Nassibu Abdul ’Diamond’. 

Mwanamuziki huyo mkongwe alianza kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye miaka ya 1960 ambapo mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya Nuta Jazz na Mlimani Park.

Alidumu na Mlimani Park mpaka mwaka 1985 na kuhamia Safari Sound aliyofanya nayo kazi mpaka mwaka 1990 na kujiunga na Msondo Ngoma mpaka sasa alipoamua kutangaza rasmi kustaafu kazi hiyo ya Kimuziki.

MARAIS WASTAAFU ALHAJI ALHASAN MWINY NA BENJAMIN MKAPA WAHUDHURIA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE MJINI HARARE.


Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Harare, Zimbabwe, kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika leo.
 Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiwasili katioka Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Harare, Zimbabwe, walikoalikwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika leo.
Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiwasili katioka Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Harare, Zimbabwe, walikoalikwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika leo. PICHA NA IKULU