Monday, April 14, 2014

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AWAASA WANAFUNZI WA KIKE UDOM KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA NGONO



Na John Banda, Dodoma
WASICHANA wasomi wa vyuo vikuu wametakiwa kujiepusha na uhuni wa
kingono na badala yake wazingatie malengo yaliyowapeleka masomoni ili
kuepuka kuzitia hasara familia zao na taifa kwa ujumla
Haya yalisemwa na Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma Kikwete alipokuwa
azindua Kongamano la wanafunzi wasichana wa Vyuo vikuu lilofanyika
Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM] juzi
Salma alisema kumekuwa na tabia ya wasichana wa vyuo vya elimu ya juu
kuwa na wanaume watatu kwa wakati mmoja ambao wao huwaita moja wa
pamba yaani mavazi, mwengine ni wa kumsaidia darasani kimasomo na
mwingine wa ukweli yaani anayempenda huku wakijidanganya kuwachuna na
kumbe wanachunwa wao kutokana na kila mtu kuwa na nguvu yake wakati wa
tendo
 Salma alisema wasichana hao wanatakiwa kujua wapo masomoni kwa
malengo maarumu ya kuzisaidia familia, jamii zinazowazunguka na taifa
kwa ujumla mara baada ya kumaliza masomo yao hivyo wanatakiwa
kujiepusha na starehe zisizo maana zinazotokana na kujirahsisha.
Mke huyo wa Rais mwenye fani ya ualimu aliwataka wasichana hao
kuhakikisha wanajitambua kama ni wanawake wenye maumbile tofauti na
wanaume  na hivyo kuhakikisha wanaiweka miili yao kuwa katika uthamini
mara baada ya kuvunja ungo kinyume cha hapo ni mimba na magonjwa ya
ngono.
Aliwafananisha wasichana na madini aina ya Lulu yanayopatikana ndani
ya samaki chaza anaishi miambani kwenye kina kilefu cha bahari na
hivyo kutokana na ugumu wa upatikananaji wake mara nyingi ilikuwa
ikitumiwa na wake wa wafalme  pekee.
''Wasichana zitunzeni Lulu zenu kwaajili ya manufaa yenu ya baadae
acheni tabia za  kujihusisha na ngono, ni lazima mjua kwamba familia
zimejifunga mkanda kukusomesheni ili mje kuzisaidia hivyo wanaume
mliokutana nao vyuoni mjue kabisa sio hao watakao kuwa wenzi wenu
katika maisha wanawapotezea muda wa masomo bure'', alisema
Aidha Mama Kikwete Aliwaambia wasomi hao wa kike wa vyuo vikuu kuwa
wanatakiwa kuwa na tabia njema ambayo itawafanya wapate mafanikio
katika kila Nyanja watakazopitia na hatimae kuwa viongozi wazuri wa
familia na taifa hili.
Salma alizindua Kongamano hilo lililoandaliwa na Wanafunzi wa chuo
Kikuu cha Dodoma lilivikutanisha vyuo vikuu vya Serikali za Mitaa,
Madini, Mtakatifu Yohana, CBE na Mzumbe walikuwepo Dodoma kutembelea
Bunge la bajeti na wiki ijayo anatarajia kuzindua mpango wa upimaji na
matibabu ya salatani ya shingo ya uzazi kwa wanawake Wilayani Bahi
leo.
Salma Kikwete akilisakata Rhumba pamoja na wanafunzi wa kike wa vyuo
vikuu waliokutana kwa ajili ya kongamano lililofanyika katika ukumbi
wa chimwaga uliopo katika Chuo Kikuku cha Dodoma [UDOM].

Prof Anna Tibaijuka akiongea na mke wa Rais Salma Kikwete mara baada
ya kuwasili katika ukumbi wa chimwaga kwenye kongamano la wanafunzi wa wakike wa vyuo vikikuu.

PICHA NA JOHN BANDA

Sunday, April 13, 2014

MAFURIKO DAR ES SALAAM KAMA BANGLADESH.


Chini na juu ni lori la mafuta likiwa limetumbukia eneo la Mbagala.
 Hatariiii......
 akijitutumua kupita lakini aaaah wapi, safari iliishia hapa.
 Hapa ni maeneo ya Kariakoo...
 

MKATABA WA MUUNGANO HAUNA SAHIHI YA NYERERE WALA KARUME-TUNDU LISU

tund_1_815d2.jpg
Mjumbe kutoka Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu  akiwasilisha maoni ya wachache  Kamati hiyo kwenye kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.

Thursday, April 10, 2014

TASAF KUZIFIKIA KAYA MILIONI 1.2 KATIKA AWAMU YA TATU.

NA JOHN BANDA DODOMA
JUMLA ya kaya milioni 1.2 zinatarajiwa kufikiwa na mpango wa Serikali wa kupitia  TASAF awamu ya tatu   (TASAF III) kwa lengo la kunusuru kaya masikini katika  wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
 Akizungumza kwenye warsha ya kutoa uelewa Madiwani,na watendaji wa Halmashauri hiyo  ,Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF ,Zuhura Mdungi  alisema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 katika awamu mbili za miaka mitano mitano.
 Alisema,mpango huo umelenga kuzifikia kaya  milioni 1.2 ambazo zinaishi katika hali masikini.
" Utekelezaji wa mpango huu unahitaji uwekezaji mkubwa kwenye mifumo na kujenga uwezo katika ngazi zote...,utatekelezwa kwa kuanza na maeneo machache na kuongeza maeneo zaidi kadri uwezo unavyojengeka na utekelezaji unavyoendelea." alisema Zuhura
 Akielezea kuhusu madhumuni ya mpango,Zuhura alisema,ni kuwezesha kaya masikini sana kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu,kuwezesha kuwa na matumizi wakati wa hari na kuwekeza kwenye rasilimali watu hususan kusomesha watoto.
 Madhumuni mengine ni kuimarisha shughuli za kuongeza kipato na kuongeza matumizi ya huduma za jamii.
Vile vile alisema,mpango wa kunusuru kaya masikini umeganyika katika maeneo mbalimbali ambayo ni kutoa  ruzuku kwa kaya masikini sana hususan zenye wajawazito na watoto ili ziweze kupata huduma za elimu na Afya lakini pia kutoa ajira kwa kaya hizo masikini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa majanga mbalimbali.
 Alisema ,eneo  lingine  la  mpango huo ni kuongeza kipato kwa kaya masikini kupitia uwekaji akiba na shughuli za kiuchumi ili kuboresha maisha,kujenga na kuboresha miundombinu inayoenda sekta za elimu,Afya na maji lakini pia kujenga uwezo katika ngazi zote za utekelezaji.
 Mpango huu Kitaifa ulizinduliwa Februari 2013 na Rais Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma.
Madiwani, Watendaji wa kata na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Chamwino Dodoma wakifuatilia jambo wakati walipokuwa kwenye Warsha ya
kujengewa uelewa kuhusu mpango wa Serikali wa TASAF Awamu ya tatu.


MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KIKAO CHA RCC DODOMA.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DKT Rehema Nchimbi kitoa maelekezo kwa watendaji hao wakuu wa serikali ngazi za Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wiliya ya Kondoa Hamis Mwenda akifafanua
jambo wakati alipokuwa akichangia jambo wakati wa kikao cha ushauri
cha mkoa wa Dodoma [RCC]