NA JOHN BANDA DODOMA
JUMLA ya kaya milioni 1.2
zinatarajiwa kufikiwa na mpango wa Serikali wa kupitia TASAF awamu ya
tatu (TASAF III) kwa lengo la kunusuru kaya masikini katika
wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Akizungumza kwenye warsha ya
kutoa uelewa Madiwani,na watendaji wa Halmashauri hiyo ,Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa TASAF ,Zuhura Mdungi alisema mradi huo unatekelezwa
kwa kipindi cha miaka 10 katika awamu mbili za miaka mitano mitano.
Alisema,mpango huo umelenga
kuzifikia kaya milioni 1.2 ambazo zinaishi katika hali masikini.
" Utekelezaji wa mpango huu
unahitaji uwekezaji mkubwa kwenye mifumo na kujenga uwezo katika ngazi
zote...,utatekelezwa kwa kuanza na maeneo machache na kuongeza maeneo zaidi
kadri uwezo unavyojengeka na utekelezaji unavyoendelea." alisema Zuhura
Akielezea kuhusu madhumuni ya
mpango,Zuhura alisema,ni kuwezesha kaya masikini sana kuongeza matumizi muhimu
kwa njia endelevu,kuwezesha kuwa na matumizi wakati wa hari na kuwekeza kwenye
rasilimali watu hususan kusomesha watoto.
Madhumuni mengine ni
kuimarisha shughuli za kuongeza kipato na kuongeza matumizi ya huduma za jamii.
Vile vile alisema,mpango wa kunusuru
kaya masikini umeganyika katika maeneo mbalimbali ambayo ni kutoa ruzuku
kwa kaya masikini sana hususan zenye wajawazito na watoto ili ziweze kupata
huduma za elimu na Afya lakini pia kutoa ajira kwa kaya hizo masikini zenye
watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa majanga mbalimbali.
Alisema ,eneo lingine la mpango huo ni
kuongeza kipato kwa kaya masikini kupitia uwekaji akiba na shughuli za kiuchumi
ili kuboresha maisha,kujenga na kuboresha miundombinu inayoenda sekta za elimu,Afya
na maji lakini pia kujenga uwezo katika ngazi zote za utekelezaji.
Mpango huu Kitaifa
ulizinduliwa Februari 2013 na Rais Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma.
Chamwino Dodoma wakifuatilia jambo wakati walipokuwa kwenye Warsha ya
kujengewa uelewa kuhusu mpango wa Serikali wa TASAF Awamu ya tatu.
No comments:
Post a Comment