Sunday, October 6, 2013

CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA CHANG'OMBE MKOANI DODOMA WAZINDUA OFISI YAO RASMI



Katibu wa CCM mkao wa Dodoma Albart Mgumba akikata utepe kuzindua ofisi za chama hicho kata ya  Chang'mbe iliyopo chang'mbe Magharibi huku viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya mkoa, wilaya na kata.



Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Drt David Malole akiwa na viongozi wa CCM kata ya Chang'mbe walipokuwa wakimsubili Mgeni Rasmi kwa ajili ya kuzindua ofisi ya chama hicho kata ya Chang'ombe na baadae kuwahutubia wananchi.



Katibu wa CCM Mkoa Albart Mgumba akimtambulimbulisha Katibu wa umoja wa wanawake wa chama hicho [UWT] Kaundime Kasasi ambaye pia ni Mama Mzazi wa Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa kwa wananchi wa kata ya Chang'ombe, kabla ya kuwahutubia wananchi hao.



Diwani wa Kata ya Chang'mbe Bakari Fundikila mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea Katika manispaa ya Dodoma akiwa kwenye Pikipiki ya mataili matatu maarufu kama bajaj yenye mashine yenye dawa ya kuulia mazalia ya mbu ambayo wameikabidhiwa miezi 2 iliyopita baada ya kukwama kusikojulikana baada ya kutolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Tangu mwaka 2011 kabla ya yeye kuwa Diwani 



Jengo la ofisi ya CCM linavyoonekana baada ya kukamilika kwaajili ya matumizi kama linavyoonekana.

katibu wa ccm mkoa wa dodoma akisalimia

Saturday, October 5, 2013

GAME YA SIMBA NA RUVU SHOOTING IMEMALIZIKA UWANJA WA TAIFA KWA SIMBA KUKUBALI KUBANWA MBAVU NA KUTOKA SARE YA 1-1.


 Mshambuliaji wa Simba, Haruna Chanongo akichuana na beki wa Ruvu shooting, stephano Mwasyika.
 Amri Kiemba akichuana beki wa Ruvu Shooting, Abuu Hashim.
 Hekaheka katika lango la Ruvu Shooting.
 Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Golikipa wa Ruvu Shooting, Abdul Seif akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Berntram Mombeki akiruka daruga la beki wa Ruvu Shooting, Abuu Hashim

Friday, October 4, 2013

MH KAGASHEKI AONGOZA MATEMBEZI YA KILOMETA 4 YA SIKU YA TEMBO DUNIANI JIJINI ARUSHA.

  Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya Tembo hao
  Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akionesha moja ya vibao ambavyo vinawaonesha Tembo wakati wa Matembezi hayo ya amani.
 Kutoka kushoto ni Mrs. Tibaijuka akifuatiwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki,Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Willbert Chambulo, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo

REDDS MISS TANZANIA AWASILI NYUMBANI DODOMA KWA KISHINDO-MKUU WA MKOA WA DODOMA DR REHEMA NCHIMBI AMPONGEZA.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa ameshika kipande cha keki  kumlisha Happiness Watimanywa kama ishara ya kumpongeza kwa kushinda taji la Redds Miss Tanzania 2013 akiwa mshiriki kutokea Dodoma kwenye mashindano ya mwaka huu.


Redds miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa akikata keki tayari kuwalisha wageni waliojitokeza kwenye hafla ya chakula cha jioni ya kumpongeza kushinda taji hilo, hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki kwenye hoteli ya Dodoma.

Tuesday, October 1, 2013

MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA AFUTIWA KESI YA UCHOCHEZI.

Kesi ya Uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mbunge Lema imefutwa!

Upande wa mashitaka, Jamhuri imeiomba Mahakama kufuta kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mhe. Lema. Hii ni ile kesi ya kudaiwa kuchochea vurugu Chuo cha Uhasibu Arusha. 
BAADA YA KUFUTWA KESI HIYO LEMA ANASEMA:
 "Nimeshinda kesi tena! Kwa kweli Mungu anatupenda sana na tutaendelea kupambana kutafuta haki bila hofu. Miili yetu na nafsi zetu zimepoteza maumivu kwa sababu ya mateso yaliyojaa uongi na hila. Hata hivyo tutaendelea na kelele za kupigania haki bila kurudi nyuma huku uvumilivu ukiwa nguzo yetu kuu" alisema Mbunge Lema ,
 katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha mara baada ya kushinda kesi dhidi yake na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo zikihusisha kilichodaiwa kuwa uchochezi kwa wanafunzi wa Uhasibu Arusha wamzomee Mulongo na kufanya fujo... Kesi hiyo imefutiliwa mbali baada ya washitaki kuomba hivyo pamoja na kwamba leo ndio ilikuwa siku ya kuanza kusikiliza ushahidi wa Mkuu wa Mkoa, Dean of Students, Makamu Mkuu wa Chuo na Maofisa wa Polisi wakiongozwa na OCD Muroto