Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa
Watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa
Chimwaga mjini Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata
utepe katika vitabu hivyo vya taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa
watumishi wa umma alivyopokea kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika
Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. Katikati ni Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan na wakwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) Profesa Idris Kikula.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa kitabu cha Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa
watumishi wa umma alivyopokea kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika
Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. Katikati ni Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan na wakwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) Profesa Idris Kikula.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinyanyua
juu Taarifa na vitabu vye majina 9,932 ya watumishi wenye vyeti vya
kugushi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata
utepe na kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi zaidi ya 9,932
waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi mara baada ya kupokea Taarifa ya
zoezi la uhakiki wa vyeti kwa
watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa
Chimwaga mjini Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
majina hayo pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi hao wa umma ambao wamegushi vyeti vyao .
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma
jina mojawapo la mtumishi aliyegushi cheti katika taarifa hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiangalia vitabu vyenye
majina ya watumishi wa Umma zaidi ya 9,932 waliogushi vyeti vyao vya
elimu ya Sekondari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,
Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
bora Angela Kairuki wakiminya kitufe kuashiria maadhimisho ya miaka 10
ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
viongozi mbalimbali, wanafunzi wa UDOM, pamoja na watumishi wa Umma
mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa
watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa
Chimwaga mjini Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akagana na
watumishi mbalimbali wa umma, viongozi pamoja wanafunzi wa UDOM mara
baada ya kumaliza kuhutubia katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia katika hadhara hiyo katika Chuo kikuu cha Dodoma UDOM.
Wanafunzi
wa UDOM wakisikiliza kwa makini Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
maadhimisho ya miaka 10 toka kuanzishwa kwake.
Baadhi
ya viongozi mbalimbali wakifatilia kwa makini Hotuba iliyokuwa
ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli katika maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo cha UDOM toka kuanzishwa
kwake.
Baadhi
ya Makatibu wakuu pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifatilia
kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Chimwaga mkoani
Dodoma.
Baadhi ya Makatibu wakuu pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafunzi pamoja na walimu wa UDOM
wakipiga makofi wakati wakimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwasili katika ukumbi wa
Chimwaga mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Ukumbi wa Chimwaga.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya
miaka 10 ya Chuo kikuu cha Dodoma UDOM katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment