Miongoni mwa manusura 22 wa ajali ya basi la Majinja lenye namba za usajili T438 CED wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa Iringa kwa matibabu. Abiria 42 wamepoteza maisha katika ajali hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Asas Abri (kulia) akiwa na viongozi wengine wakiwajulia hali manusura wa ajali hiyo.
Kontena lilokuwa limepakiwa katika lori la mizigo Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja.
Kontena lilokuwa limepakiwa katika lori la mizigo Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja.
Kontena likiwa limelalia basi
Kontena likiwa limelalia basi
Foleni ya magari katika eneo la Changarawe baada ya ajali hiyo.
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Basi likiwa limelaliwa
Basi likiwa eneo la tukio
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Basi likiwa limelaliwa
Basi likiwa eneo la tukio
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (wa pili kulia) akiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ,Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Iringa Salim Asas Abri (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita eneo la ajali
Hivi ndivyo Basi la Majanja linavyo onekana mara baada ya kuondoa Lori lilikuwa limekandamiza basi hilo.
Umati wa watu mbalimbali wakiwemo wasafiri wasafiri waliokuwa katika mabasi mengine wakiwa wamejaa kushuhudia Ajali hiyo.
Shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea
Simanzi ilitawala katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga wakati maiti zilizopatikana kwenye ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,zikiwasili.
Zaidi ya 45 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ni majonzi kwa kila alefika kwenye hospitali hii.
Sehemu ya Wasamalia na Mafundi waliosaidia kazi ya kuyatenganisha magari hayo wakiangalia kama kuna watu waliosalia kwenye basi lililopata ajali leo kwa kugongana na kuangukiwa na lori la Mizigo.
Lionekanavyo basi hilo kwa nyuma.
Basi hilo linavyoonekana baada ya ajali hiyo ambayo imeleta majonji makubwa sana kwa Taifa.
Kontena la Lori hilo likiwa limewekwa pembeni baada ya kuondolewa kwenye eneo la Ajali.
Muonekano wa Basi la Abiria na Lori yaliyo athirika kwa ajali hiyo
Mashuhuda
Basi la Abiria likiwa katika Hali mbaya baada ya ajali
Waokoaji wakiwa wanaendelea kufanya ushirikiano namna ya kuwasaidia watu waliopata ajali hiyo.
Miongoni mwa watu wakiwa wanatazama namna Magari hayo yalivyopata ajali
Askari wa usalama Barabarani wakiwa wanahakikisha watu mbalimbali waliodhurika katika ajali hiyo wanaweza kupata msaada/huduma kwa haraka.
Basi lililokuwa limebeba abiria waliokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar es salaam Lenye namba za usajili T438 CDE likiwa katika hali mbaya.
Watu 42 wamefariki maeneo ya Changalawe mji mdogo wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya basi la abiria lililokuwa likitokea mkoani Mbeya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limetokea Dar es Salaam.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema tukio hilo limetokea leo majira ya 09:30 asubuhi ikihusisha basi namba T:438 CDE likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam na lori aina ya Scania namba T:689 APK lililokuwa likiendeshwa na dereva Sebastiani Mgama likitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa kati ya watu 42 waliofariki kwenye ajali hiyo wanaume ni 33,wanawake 6 na watoto 3 huku maiti nane zimeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa kwa ajili ya shughuli za mazishi.
Aidha amesema maiti hizo zilihifadhiwa kwa muda katika kituo kidogo cha afya cha Mafinga na kisha kuhamishiwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi 22 wa ajali hiyo ambapo waliojeruhiwa kidogo wataendelea kupata matibabu katika kituo cha afya cha mji mdogo wa Mafinga.
Kamanda Mungi amesema kuwa katika eneo hilo kuna bonde na uchakavu wa barabara,kutokana na mwendo kasi wa dereva wa lori ambaye alikuwa akijaribu kulikwepa shimo lililokuwa katikati ya barabara kabla ya kupishana na basi la abiria.
Amesema kufuatia hali hiyo ikasababisha kupoteza mwelekeo kisha kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo kuliangukia basi la abiria ambalo kwa muda huo lilikuwa karibu na lori hilo.
Hata hivo Kamanda Mungi amesema taarifa zaidi zitatolewa kesho Machi 12 ,2015 ambapo pia ametoa wito kwa wamiliki wa magari na madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
MAJINA YALIYOPATIKANA YA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BASI HILO HADI SASA NI: Baraka Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.
Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule.
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.
No comments:
Post a Comment