Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akiwaagiza
viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chang’ombe kuhakikisha wanakamilisha
ujenzi wa maabara sekondari ya Lukundo ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe.
Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wa Maabara Manispaa ya Dodoma wakati
alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Feb. 16, 2015.
Tuesday, February 17, 2015
MHE. CHIKU GALLAWA AKAGUA UJENZI WA MAABARA MANISPAA YA DODOMA, AMUAGIZA MKURUGENZI KUWACHUKULIA HATUA WATENDAJI WANAOSHINDWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MAABARA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa
(mwenye kilemba kichwani) akimsikiliza Afisa Mtendaji wa Kata ya Msalato
Dodoma Ndg. Herman Malindira
(kulia) akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi maabara kwenye sekondari ya
Chikole Feb. 16, 2015.
Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akitoa maagizo
kwa viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Msalato baada ya kutoridhishwa na
maendeleo ya ujenzi wa maabara wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara
Mjini Dodoma Feb. 16, 2015.
Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akionesha
kutokuridhishwa na hatua ya ujezi wa maabara kwenye sekondari ya Miyuji
inayojengwa na Kata za Miyuji na Mnadani ikiwa hatua ya msingi wakati
alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015, Amemuagiza
Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma kuwachukulia hatua watendaji wote walioshindwa
kusimamia ujenzi wa maabara.
Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akiwaagiza
viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chamwino kufanya kazi kwa
kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakamilisha ujenzi
wa maabara sekondari ya Chinangali ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe.
Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa
Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015 na kukuta maabara ik kwenye hatua ya ujenzi
wa msingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment